Wednesday 11 February 2015

BOBBI KRISTINA 'KUFA' SIKU MOJA NA WHITNEY

http://img2.timeinc.net/people/i/2013/news/130722/bobbi-kristina-600.jpg


Familia ya Bobbi Kristina Brown watachomoa mashine 
yake ya kupumulia siku ya Jumatano ili Brown
 aweze kufa siku ileile aliyokufa mama yake 
Whitney Houston, gazeti la New York Post limeripoti.

Bibi yake Brown na mama yake Whitney,
 Cissy Houston, alipendekeza wazo hilo mwishoni
 mwa juma , kulingana na the Post.
 


Familia inapanga kuchomoa mashine ya kupumulia
 usiku wa Jumanne kuingia Jumatano.


Brown, mwenye umri wa miaka 21, amepooza
 tangu alipokutwa kwenye bafu
 nyumbani kwake huko Georgia, Januari 31.

Polisi wanafanya uchunguzi, wakimfutailia 
zaidi mpenzi wake Nick Gordon, aliyemkuta kwenye bafu hilo. 


Inaripotiwa Brown alikuwa na majeraha usoni alipokutwa.

Whitney Houston alifariki dunia Februari 11, 2012,
 baada ya kuzama kwenye bafu 
lililojaa maji na baadae mwili wake ukikutwa na dawa
 za kulevya.

Familia yake na marafiki, akiwemo baba yake
 Bobbi Kristina, Bobby Brown, wameandaa sala
 ikiambatana na mishumaa siku ya Jumatatu 
huko Riverdale.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!