Tuesday 10 February 2015

AJIRA: TANGAZO LA KAZI KWA WATAALAM WA AFYA (MKAPA FELLOWS)



Katika kuchangia jitihada za Serikali za kuboresha utoaji na upatikanaji wa huduma bora za afya, Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/AIDS (BMAF) imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali tokea mwaka 2005, ukiwemo mradi wa ‘Mkapa Fellows’. 


Kuanzia Januari 2013, Taasisi inatekeleza Mradi wa Mkapa Fellows awamu ya pili wenye madhumuni ya kuimarisha huduma za afya, kupitia ufadhili wa Serikali ya Tanzania, Serikali ya Ireland (Irish aid), Shirika la ACACIA na Makampuni binafsi mbalimbali, Mashirika ya Umma na Watu Binafsi.
Mradi huu una lengo la kuongeza wataalam wa afya, ili kuimarisha huduma za UKIMWI pamoja na Afya ya mama na mtoto katika Halmashauri zilizopo maeneo yenye uhaba mkubwa wa watumishi kutokana na changamoto ya mazingira yake. Katika awamu ya kwanza ya mradi huu ( 2013- 2014), wataalam wa afya 32 waliajiriwa na kupangiwa kazi katika Halmashauri ( kwenye mabano) zilizopo katika Mikoa ya Rukwa (Sumbawanga vijijini, Kalambo na Nkasi), Shinyanga (Kahama na Kishapu) na Kagera (Biharamulo).
Awamu ya pili (2015-2017) inakusudia kutekeleza mradi huu katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu, ambapo Taasisi iko katika mchakato wa kuajiri watumishi wa Afya 33 kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali hapa chini:

****DOWNLOAD THE ATTACHMENT BELOW****

Izingatiwe kwamba:
• Ajira ndani ya mradi huu wa Mkapa Fellows II itatolewa kwa mkataba wa miezi kumi na nane (18) na mara baada ya kukamilika kipindi hiki, waajiriwa wote katika mradi huu watatakiwa kujiunga katika Utumishi wa Umma kulingana na taratibu na kanuni za Serikali za Ajira;
• Watumishi walioajiriwa katika Utumishi wa Umma, au katika Taasisi/Vyuo vya mashirika ya dini (FBOs) hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi;
• Wataalamu wenye umri chini ya miaka 43 ndio wanaoshauriwa kuomba nafasi hizi za kazi, na watakuwa na fursa ya kupata ajira Serikalini kwa masharti ya kudumu na pensheni mara baada ya kukamilika kwa ajira ya mkataba
Waajiriwa wote (Fellows) katika Mradi huu watapata mafao yafuatayo:
• Mishahara kulingana na ngazi zilizoainishwa katika Mradi ;
• Posho ya nyumba, mafunzo kazi pamoja na ‘‘laptop’’ kompyuta
• Mafao ya matibabu
• Kiinua mgongo baada ya kumaliza miezi 18 ya mkataba
• Baada ya kukamilisha kipindi cha mkataba watakuwa sehemu ya ‘‘Mkapa Fellows Alumni’’
Maombi yote yaambatanishwe na:
1. Barua ya maombi ya kazi, ikipendekeza Halmashauri mwombaji anayopendelea kufanyia kazi, na pia aonyeshe ridhaa ya kujiunga na Utumishi wa Umma, baada ya mkataba wa miezi 18 kumalizika.
2. Nakala ya cheti cha Taaluma na Cheti cha kidato cha 4 na 6 (iwapo anacho), na viwe vimethibitishwa na Hakimu au Wakili
3. Picha mbili (2) – saizi ya Pasipoti na maelezo binafsi (CV), ikionyesha umri, anuani kamili na namba ya simu ya kiganjani, pamoja na anuani/ namba ya kiganjani ya wadhamini wako wasiopungua wawili.
Mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe 23 Februari 2015

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!