
Ngoja niongee tena na waajiriwa leo..
Je, unawafahamu hawa jamaa wawili kwenye hii picha?
Ungeokota picha hii
barabarani ungeweza kudhania ni kina nani?
Huenda ungefikiri ni watu tu
kama wewe sema tu huwajui kama wao wasivyokujua. Au siyo?
And you would
be right! Lakini pengine ungekuwa hujui kuwa hawa jamaa wawili wana
influence juu ya maisha yako pengine ya kila siku sasa hivi!
Ladieees and Gentlemen, my honour to introduce to you ndugu BRIAN ACTON
hapo kushoto and ndugu JAN KOUM hapo kulia.. Do these names ring the
bell? No? Ok. Hawa ndiyo waanzilishi wa 'mtandao' wa WatsApp miaka
takribani 6 tu iliyopita in 2009!
Na sasa ni mabilionea. In just 6 years.
Na sasa ni mabilionea. In just 6 years.
Akili ya mwanadamu yeyote Mungu aliiumba kwa "akili" sana yaani! Sema
tu akili zingine zinaamuaga kuchungulia upande wa pili kukoje na zingine
zinaamua kubakia hivyo hivyo ndani ya "fence".
Ukitaka ujue akili yako iko katika kundi lipi basi upate matatizo ndo kipimo cha kujua unawazawazaje!
Kama wewe una comfortable life toka utotoni yaani ukikohoa tu dakika sifuri mko Agakhan kuchek afya hebu sasa jaribu kujipa matatizo angalau madogo madogo.. kama kwenda sehemu bila nauli ya kurudia uone wewe unawazaje kichwani.
Utaweza kurudi? Utapata option ngapi za kusolve ishu
ya nauli ya daladala kwa mfano. Wengine watasema huo ni uchizi.
Hahaaaa. Basi sawa.
Sasa bana hawa jamaa wamesoma kiasi kama
wewe labda, umewazidi usikute. Hawa jamaa walikuwa waajiriwa kama wewe.
Waliajiriwa na kampuni moja maarufu kweli kweli siyo tu huko kwao bali
dunia nzima. Yahoo!
Kuna mtu anayesoma hapa hajui Yahoo! ?
Huyo mrefu kabla ya Yahoo alifanya kazi pia Ernst & Young!
So.. Walipiga kazi hapo Yahoo! kwa takribani miaka 10! Mwenye Yahoo
alikuwa bilionea wao walikuwa wafanyakazi wa bilionea. Kumbe hawakujua
kuwa wao nao walikuwa ni mabilionea tena zaidi ya bilionea aliyekuwa
kawaajiri.
Siku walipojitambua wakaacha kazi Yahoo! Unajua kuacha kazi Yahoo inahitaji uvute pumzi kwenye mapafu mara tatu tatu. Au nakosea. Nadhani kuacha kazi "Juakali Enterprises" ni rahisi kuliko kuacha kazi Yahoo. Imagine kama hapo ulipo tu sasa hivi kuacha kazi haijawahi kukujia akilini je ungekuwa Yahoo?
Kufumba na kufumbua hao wakaibuka na kitu cha WATSAPP mwaka 2009. Tena ilianza kama free app then ndo wakaweka tozo kidogo ili kucontrol ukuaji wa kutisha wa WatsApp!!
Boooy!
Hivi Unajua ndo maana
wengine Mungu huwa sometimes anachafua hali ya hewa kazini kwako ili
utoke ukawe tajiri huko nje. Wewe kesho yake unaanza maombi ya kufunga
na kuhamishwa bosi. Wanasema Mungu si "Asumani".
Wiki haifiki bosi
kahamishwa. Unapeleka ushuhuda kanisani bila kujua kule mawinguni Mungu
anakuangaliaaaaa.. Halafu anakuacha kama ulivyo. Unabaki na utajiri
mkubwa kichwani mwako umeufungia kwenye Yahoo yako. Iangalie Yahoo yako
vizuri. Usijekuta kuna WasApp yako miaka miwili tu mbele yako.
Hawa jamaa wakaanzisha WatsApp yao ikagrow then mwaka jana tu FACEBOOK ikaamua kuwanunua kwa USD 19 BILLION. Si una calculator. Ni trilioni ngapi za bongo? Wangekuwa bado wako Yahoo je.
Itazame upya Yahoo yako usikute inakufungia utajiri mkubwa tu.
Sasa hivi ni board members wa Facebook. Na shares juu. Yaani hivi unavyosoma hii post hapa fb wao wanaingiza hela hivo.
Cha ajabu walipoacha kazi Yahoo wakiwa likizo bado wanawaza wafanye
nini hasa, waliapply kazi Facebook wakapigwa chini wote. Huyo Acton
akaona isiwe tabu Facebook 'kitu gani' akaapply TWITTER nako akakosa!
Dah. Unajua sometime ukiwa karibu "kutoka" kimaisha ndo vishawishi vya
kurudi maisha yako ya zamani (mfano kuajiriwa) huwa vinashika kasi kweli
kweli.. Wakati mwingine Mungu atakukosesha kazi nzuri qualifications
unazo na experience unayo lakini unakosa kazi. Mungu anajua..
usilalamike tu ooh niliapply sehemu mbili nikakosa Mungu anataka utumie
akili yako banaa..
Sasa Mfano wangepata kazi Facebook ingekuwaje? Wangekuwa na hisa za Facebook leo kweli?
By mwezi wa nne mwaka jana (2014) WatsApp ilikuwa na Active Users milioni 500 kwa mwezi na kila siku kulikuwa na picha milioni 700 na video milioni 100 watu wanazoshare watsapp kila siku mpaka mwaka jana mwezi wa nne. Imagine mwezi wa nne mwaka huu itakuwaje?
By mwezi wa nne mwaka jana (2014) WatsApp ilikuwa na Active Users milioni 500 kwa mwezi na kila siku kulikuwa na picha milioni 700 na video milioni 100 watu wanazoshare watsapp kila siku mpaka mwaka jana mwezi wa nne. Imagine mwezi wa nne mwaka huu itakuwaje?
Watumiaji wa
WatsApp kwa siku ilikuwa watu 833,000! (India ikiwa ndo inaongoza kwa
kutumia WatsApp duniani). Mtu yuko Marekani hela zinatoka India na kila
kona ya dunia. Wewe uko Magomeni hela hata ya Ubungo tu hupati. Mpaka
uende hapo Yahoo ulipoajiriwa. Buni basi hata kitu tu cha ziada. Yahoo
siyo mbaya wewe tu unaichukuliaje. Kwamba umefika au unapita?
So
my friend. Narudia tena, ingalie upya Yahoo yako. Miaka 10 bado upo hapo
"Yahoo" umeufungia utajiri humo kwa mwajiri wako. Unazidi kuogopa
kutoka. Tafakari vizuri.
You are probably 5 times richer than your
employer's worth.
And 10 times richer in the next 10 years.
But not if you will still be on that desk.
But not if you will still be on that desk.
Hakuna tajiri aliyeajiriwa.
Ila kuna mabilionea lukuki bado wako "Yahoo"!
Ila kuna mabilionea lukuki bado wako "Yahoo"!
Asante sana.
KWA MAWASILIANO PIGA NAMBA: +255 783 149 561
Email: ally.shaaban@yahoo.com
DAR ES SALAAM, TANZANIA.
DAR ES SALAAM, TANZANIA.













No comments:
Post a Comment