Tuesday 27 January 2015

WATOTO WANNE WA FAMILIA MOJA WAFA BAADA YA KULA CHAKULA CHENYE SUMU MKOANI KIGOMA

Watoto wanne wa familia moja wakazi wa kijiji cha kibambila wilayani kakonko mkoani kigoma wamefariki dunia na mmoja amelazwa katika kituo cha afya kakonko baada ya kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu .



Mganga  mkuu wa wilaya ya kakonko Dk. Fadhil Seleman  amewataja watoto hao waliofikishwa kituo cha  afya kakonko kuwa ni  Neema Joseph, Jonas Joseph, Majaliwa Joseph, Yusuph Joseph wote wakiwa na umri wa kati ya miaka 11 na 18 walifikishwa hospitalini hapo  wakiwa na hali mbaya na walipoteza maisha wakati wanaendelea kupatiwa huduma na kwamba uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa watu hao wamekula sumu katika ugali.
 
Akizungumzia tukio hilo baba wa watoto hao Joseph Kajolo ambaye alinusurika katika tukio hilo amesema hajui chanzo cha tukio hilo huku baadhi ya wananchi wa kakonko waliokuwa wakieleza maskitiko yao nakusema  vitendo hivi vimekuwa vikijirudia mara kwa mara katika wilaya hiyo.
 
Mkuu wa wilaya kakonko Peter Toyima amesema polisi inamshikilia mtu mmoja kuhusiana na tukio hilo huku akiwataka wananchi kuacha vitendo vya kuwekeana sumu.

1 comment:

Anonymous said...



aziz bilal18:11


1


Kila siku mapya nchini mwetu,mara kuuliwa albinos,mara kuuwawa mwenyekiti wa kijiji na viungo vyake kupikwa na kuwekwa ktk masufuria na leo mpya sana ni kuwekeana sumu ktk chakula.Sijui yataisha lini?.

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!