Tuesday 27 January 2015

THRD: SAIDIENI KUKAMATWA KWA WALIOVAMIA KITUOCHA POLISI IKWIRIRI

Mtandao wa Kutetea Haki za Binadamu (THRD), umewaomba wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwasaka watuhumiwa wa ujambazi katika Kituo cha Polisi Ikwiriri.
 
Mratibu wa mtandao huo, Onesmo Olengurumwa, alisema tukio la kuvamiwa kituo hicho ni la kusikitisha kwa kuwa polisi ndiyo wanastahili kulinda raia na mali zao, lakini sasa wanashambuliwa.
 
“Jeshi la Polisi ni watetezi wa haki za binadamu, kilichotendeka hakivumiliki, tuungane na Polisi kukemea na kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wahusika,” alisema.
 
Alisema silaha zilizoporwa ni nyingi na zitaweza kutumika katika matukio mengine ya kihalifu ambayo yataharibu maisha ya Watanzania wengi zaidi, hivyo ni vyema wahusika wakakamatwa na silaha husika kurudi kwenye mikono ya Polisi.
 
Alisema raia ni sehemu ya Jeshi la Polisi, hivyo wanapaswa kushirikiana kikamilifu ili kuwaweka raia katika hali ya usalama muda wote na kwamba kukamatwa kwa watuhumiwa hao kutawezesha silaha husika kukamatwa na hivyo kupunguza matukio ya uhalifu.
 
Tukio hilo lilitokea Januari 21, mwaka huu, saa 8:00 usiku baada ya kundi la majambazi kuvamia kituo hicho na kuua askari wawili na kuiba bunduki mbili aina ya Sub Machine Gun (SMG), Semi Automic Rifle (SAR) mbili, shotgun moja, bunduki mbili za kulipulia mabomu ya machozi na risasi zaidi ya 60.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!