Pages

Saturday, 24 January 2015

RAIS KIKWETE ATEUA MAWAZIRI NANE WAPYA




Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya kikwete wa Tanzania ametangaza mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.


Rais amewateua mawaziri wanane wapya pamoja na manaibu watano.
Tangazo hilo lilifanywa na katibu katika ikulu ya rais balozi Ombeni Sefue.
Mabadiliko hayo yanajumuisha wadhfa wa waziri wa nishati na kawi wa Profesa Muhongo ambaye amejiuzulu mapema leo pamoja na wadhfa wa waziri wa ardhi ambao uliwachwa wazi baada ya kupigwa kalamu kwa Anna Tibaijuka.
Mawaziri hao wawili wanahusishwa na kashfa ya ufisadi ambayo ilimshinikiza mwanasheria mkuu pia kujiuzulu.Nafasi ya Profesa Muhongo imechukuliwa na aliyekuwa naibu wa waziri wa ardhi, George Simbachawene
Rais Kikwete amewaapisha mawaziri hao wapya hii leo katika tangazo lililorushwa hewani na runinga ya taifa moja kwa moja.

Mawaziri Kamili

George Simbachawene- Waziri wa Nishati na Madini

Mary Nagu -Waziri wa nchi Mahusiano na Uratibu

Harrison Mwakyembe - Waziri wa Afrika Mashariki.


Wiliam Lukuvi - Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi

Steven Wassira - Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika

Samwel Sitta - Waziri wa Uchukuzi

Jenista Mhagama - Waziri wa Sera na Uratibu wa Bunge

Christopher Chiza- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu 

Uwekezaji na Uwezeshaji


Manaibu Waziri


Steven Masele - Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais 


Muungano

Angellah Kairuki - Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na 


Makazi

Ummy Mwalimu- Naibu Waziri wa Katiba na Sheria

Anna Kilango- Naibu waziri wa Elimu

Charles Mwijage - Naibu Waziri wa Nishati na Madini

No comments:

Post a Comment