Leo tunalea mtoto tumemuokota mama yake kamtupa.Ameokotwa mitaa ya nyumbani kwangu kwenye majani.
Mama wa mtoto huyu kamtupa amekesha usiku kucha kwenye majani akilia mpaka sauti imekauka.Ameng'atwa na mbu kila mahali kalikuwa kamejinyea kananuka pengine hakakuoga siku tatu.
Baada ya kushiba usingizi maana amekesha manyasini.Huo uso ni mbu hizo.Mama ake alimuacha na kirambo cha nguo chafu na kipande cha sabuni ili watakaomuokota wafue nguo.
CRD: Blog ya wananchi.
1 comment:
Mwenyezi mungu atakujaaliya kwa huruma mapenzi na roho yako safi utajaaliwa kupata mengi sana hata zaidi ya huyo mtoto ningependelea jina mngemuita Blessings au Baraka.
Post a Comment