Tuesday 27 January 2015

MAUMIVU MWILINI CHANZO NA TIBA YAKE!


Maumivu mbalimbali mwilini; chanzo na tiba yake
Ishara za mwanzo kabisa za asidi kuunguzwa ndani katikati ya seli au kwa maneno mengine asidi kuzidi kwenye seli za mwili na madhara ya kijenetiki ambayo yanaweza kujionesha, ni maumivu mbalimbali yanayozidi kujitokeza katika mwili.
Kutegemea na kiasi cha asidi mwilini na namna na eneo lenyewe asidi ilipojijenga maumivu maalumu ya mwili hujitokeza. Maumivu hayo yanajumuisha;


. Kiungulia (heart burn)
. Maumivu ya moyo (angina)
. Maumivu sehemu ya chini ya mgongo (lower back pain)
. Yabisi (rheumatoid)
. Maumivu ya kichwa (migraine headaches)
. Maumivu katika kiuno
. Maumivu mbalimbali katika mishipa
. Miguu kuwaka moto
. Homa za asubuhi kwa kina mama wajawazito n.k
Watu wengi siku hizi hawawezi kuishi wiki mbili au mwezi mmoja bila kumeza aina fulani ya dawa ya kupunguza maumivu.
Ni rahisi kuelewa namna gani maumivu ambayo hayajasababishwa na ajari au maumbukizo yanavyoweza kujitokeza mwilini.
Viwanda vya madawa vinatumia mabilioni ya fedha kutafiti dawa hizi na zile za kuondoa maumivu na mabilioni mengine zaidi hutumika kutangaza aina fulani ya dawa za kuondoa maumivu.
Ili kuuelewa mfumo wa utengenezwaji wa maumivu mwililini, tunahitaji kwanza kujifunza namna usawa wa asidi na alkalini unavyofanya kazi katika mwili.
Hali ya uasidi husababisha kuunguzwa kwa baadhi ya miishio ya neva mwilini. Kunapotokea hayo, ubongo huonywa juu ya mabadiliko hayo ya kikemekali ya kimaeneo, ambayo sote hutafsiri kama MAUMIVU. Kwa maneno mengine, hali ya uasidi ndani ya mwili ndiyo hupelekea kusikia maumivu.
Masaa 24 kwa siku seli zetu ndani ya mwili zinaunguza kaboni kama mafuta (cells burning carbon) ili kutuacha katika hali joto ya nyuzi joto 37.5. Unapochoma kitu chochote, kinatoa nje taka moshi. Taka zote hizo toka katika seli zote za mwili, lazima zirekebishwe muda wote wa masaa yote 24 kwa msaada wa matunda na mboga za majani.
Kwa kawaida wakati damu yenye maji ya kutosha inapoizunguka seli, baadhi ya maji huingia ndani ya seli na kutoa nje molekuli za haidrojeni. Maji huisafisha asidi toka ndani ya seli na kuiacha sehemu ya ndani ya seli katika hali ya ualikalini ambayo ni hali yake ya kawaida na ya mhimu.
Kwa afya bora kabisa, mwili unatakiwa kubaki katika hali ya 7.4 katika kipimo cha P.H (Potential Hydrogen).
Hali hii ya 7.4 PH huhamasisha afya kwa sababu ndiyo hali inayoviwezesha vimeng’enya vinavyofanya kazi ndani ya seli ambavyo hupata ufanisi mzuri katika P.H hii. Utiririkaji wa kutosha wa maji ndani na nje ya seli huifanya sehemu ya ndani ya seli kubaki na kuhimili hali yake ya kiafya ya kiualikalini.
Ndani ya miili yetu, figo husafisha haidrojeni iliyozidi ambayo husababisha asidi toka katika damu na kuiweka katika mkojo unaozarishwa. Kadiri mkojo unavyozarishwa kwa wingi ndivyo mwili unavyojiweka katika hali ya ualikalini kirahisi zaidi. Hii ndiyo sababu mkojo unaokaribia rangi ya uweupe ni kiashiria cha kufanikiwa kwa mfumo wa uondoaji wa asidi wakati mkojo wa rangi ya njano au chungwa ni ishara ya kuunguzwa kwa asidi mwilini.
Watu wanaodhani kwenda uani kwa ajili ya haja ndogo mara mbili au tatu kwa siku ni usumbufu kwao na hivyo kuacha kunywa maji ili kuzuia hilo hawana uelewa wa namna wanavyohatarisha miili yao.
Ubongo unalindwa vizuri zaidi dhidi ya asidi kutokana na ukweli kuwa unapata umhimu wa kwanza katika kusambaziwa maji kwa ajili ya mahitaji yake yote. Sehemu zingine za mwili haziwezi kuwa na bahati hii wakati maji yanapokuwa yanapatikana kwa njia ya mgawo. Ingawa upungufu wa maji unapobaki kwa muda mrefu, ubongo pia huathiriwa kutokana na hali ya uasidi katika seli, hivyo hali kama za kupoteza kumbukumbu na magonjwa ya mishipa hujitokeza.
Maumivu ambayo hayakusababishwa na jeraha au ajari, ni kiashiria kuwa tishu, ogani, maungio na seli vina asidi iliyozidi ambayo inahitaji kufanywa alkalini.
Moja ya sababu kuu ya mtu kutakiwa kula matunda na mboga za majani kwa wingi ni kuwa vyakula hivi ni alkalini, wakati nyama, kuku, samaki, nyama ya nguruwe, chipsi, ugali, pasta/tambi, wali, mkate, mayai, maandazi, chapati, soda zote na jusi zote za viwandani zote ni asidi.
Asilimia 80 ya mlo wa mtu kwa siku inapaswa kuwa ni mboga majani na matunda na asilimia 20 ndiyo iwe vyakula vingine.
Wengi wetu siku hizi tunakula vyakula ambavyo vimekwisha andaliwa tayari katika makopo au maboksi ai migahawa (fast food) na hatutumii vyakula vyenye alkalini ya kutosha. Kumbuka kuwa kabonidayoksaidi ni asidi pia kama ilivyo kwa kahawa, chai na alikoholi ambavyo huathiri PH ya damu na tishu.
Unaweza kukinunua kipimo cha PH na ukawa unajipima P.H ya mate na mkojo wako mara kwa mara ili kupata mwelekeo wa namna gani ufanye kuitunza 7.2 mpaka 7.4 kwenye seli ndani ya mwili wako. Ikiwa mate yanasoma 6.0 au 6.5 ni kiashiria kuwa una asidi iliyozidi kwenye seli zako.
Vyakula na vinywaji vyenye Alkalini nyingi: siagi ya maziwa, mtindi mtupu, lozi, mboga za majani zenye rangi ya kijani, karoti, nyanya, kitunguu, uyoga, tango, kabeji, matunda karibu yote, maji ya limau, chai ya tangawizi, asali mbichi, mafuta ya katani na mtama.
Vyakula na vinywaji vyenye Asidi nyingi: siagi, krimu ya maziwa, ice cream, maziwa, jibini ngumu, maharage, karanga, korosho, viazi, chai ya rangi, kahawa, pombe, soda zote, juisi zote za viwandani, viongeza utamu vya viwandani, sukari, nyama, samaki, wali, ugali, pasta/tambi na biskuti.
Kwa wewe unayesumbuliwa na maumivu mbalimbali mwilini kila mara fanya yafuatayo kwa muda wa wiki 2 au mpaka utakapopona kabisa;
1. Maji: Kunywa maji glasi 8 hadi 10 kila siku. Unaweza kuamua siku 1 ukashindia maji pekee na siku inayofuatia ukala chakula hasa kama maumivu yamekuwa ni sugu na yamedumu kwa muda mrefu.
2. Matunda: Asilimia 40 ya mlo wako kwa siku iwe ni matunda. Unaweza ukaamua moja kati ya milo yako iwe ni matunda tu, mfano unaweza ukaamua ama chakula cha mchana au cha usiku kiwe ni matunda tu mpaka unashiba.
3. Mboga za majani: Asilimia 40 ya chakula chako kwa siku iwe ni mboga majani. Unaweza kufanya hivi; chukuwa ama samaki wa kukaangwa au nyama ya kukaangwa, pembeni weka sahani iliyojaa mboga majani, kula hivyo viwili mpaka ushibe bila kuongeza ugali au wali katika moja ya milo yako kama ni wa mchana au usiku.
4. Chai ya tangawizi: Chemsha chai ya kutosha ya tangawizi kama lita 2 hivi na unywe taratibu kutwa nzima huku ukitumia asali mbichi kama sukari kwenye hiyo chai, tangawizi peke yake usiongeze majani ya chai.
5. Kitunguu Swaumu: Chukuwa kitunguu swaumu kimoja na ukigawe mara 2, menya nusu yake (punje 10 au 15), menya punje moja baada ya nyingine na kisha kikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu kisha meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala au fanya kutwa mara 2.
6. Mazoezi: Inashauriwa pia kuepuka kubaki katika mkao mmoja kwa muda mrefu iwe ni kukaa au kusimama. Watu wengi kutokana na kazi wanazofanya wanalazimika kubaki wamekaa au wamesimama tu kwa masaa mengi kwa siku jambo ambalo ni hatari kwa afya kwa kuwa asidi hujikusanya hivyo kwa urahisi zaidi. Yapo mazoezi maalumu ya kufanya kila mara kwa watu wa kazi za aina hiyo ili kurudishia damu katika mfumo na hivyo kutoa nje taka za asidi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!