Kufuatia mabadiliko ya Baraza la mawaziri alilofanya Rais Jakaya Kikwete viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na Dini pamoja na wananchi wa kawaida wametoa maoni yao huku wengine wakipongeza huku mwenyekiti wa taifa wa chama cha Demokrasia na maendeleo chadema mhe Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa ukawa akisema hakuna jambo jipya kwa sababu bado sura ni zile zile.
Mh.Mbowe amesema hakuna jambo jipya katika baraza hilo kutokana na ukweli kuwa watu ni wale wale ila amebadilishwa wizara na hivyo ni sawa na kwamba hakijafanyika chochote.
Kwa upande wake mwenyekiti wa taifa wa jumuiya ya wazazi chama cha mapinduzi CCM Mh. Abdalah Bulembo amesema mabadiliko aliyoyafanya Rais ni yenye tija na kuongeza kuwa kitendo cha Profesa Sospeter Muhongo kujiuzulu ni ishara ya kukubali matokeo ili kukinusuru chama cha mapinduzi.
Naye Sheikh Rajabu Katimba ambaye ni msemaji wa jumuiya ya taasisi za kislamu amesema kujiuzulu Prof muhongo na kuteua baraza lingine siyo Dawa peke bali waliokula fedha za umma wawajibishwe.
Kwa upande wawananchi Bi.Mary Massawe na Bw .Peter Karia wamewataka viongozi waliobaki madarakani kutambua kuwa wamepewa jukumu kubwa na wajifunze kutoka kwa wenzao kwani taifa linawategemea na siyo kufanya mambo kama vile nchi haina.
No comments:
Post a Comment