Tuesday 27 January 2015

JINSI YA KUTUNZA AFYA YA KINYWA NA MENO:



Utunzaji wa kinywa na meno huimarisha afya ya kinywa,meno,fizi na huboresha mfumo wa chakula(koromeo,utumbo mkubwa/mdogo,bandama hadi njia ya kupitisha haja kubwa). Kujali inajumuisha kuswaki,kusukutua,kufanya uchunguzi mara kwa mara na kula mlo ulokamilika.



 Kutunza kinywa na meno huzuia meno kuoza,huzuia magonjwa ya fizi inayoathiri uimara wa meno na kuyazuia yasin'goke,hukufanya usihangaike kwenda kwa daktari mara kwa mara,huzuia harufu mbaya mdomoni'bad breath-halitosis',hufanya meno kuwa meupe haswa kwa wavuta sigara,hutoa mabaki ya vyakula na huongeza uwezo wa meno kuishi kwa mda mrefu kwani wengi wanapofikia umri wa utu uzima huwa wamekwishan'goka idadi kubwa ya meno na wengi huzeeka wakiwa vibogoyo,wakati wanaojali vinywa vyao huzeeka wakiwa na meno.Njia pekee ni kujali lishe bora,kupiga mswakina dawa yenye flouride(mara mbili kutwa na kusukutua walau mara tatu kutwa),epuka kula sukari,tumbaku na safisha ulimi mara kwa mara.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!