Kipindi cha katikati ya mwaka kampuni nyingi hutangaza ujio wa programu mpya au kuboresha zile za zamani.
Kwa mfano, tayari Kaspersky imeshatangaza rasmi toleo la mwaka 2015, kabla ya kufuatiwa na kampuni ya Microsoft iliyotangaza toleo la Windows 10 .
Kabla ya windows 10 kulikuwa na windows 8 na nyingine za nyuma zaidi , ila kwenye toleo la windows 8, kampuni hii haikufanya vizuri sokoni, hasa kwenye mauzo na matumizi ya bidhaa hii.
Kuna taarifa japo sio rasmi kuwa ni asilimia 20 tu ya watumiaji ya windows za nyuma kama XP na 7 ndiyo waliohamia windows 8. Inategemewa windows 10 kuziba mwanya huu .
Windows 10 ambayo kwa jina la kiufundi inaitwa ‘threshold’ yenyewe itaanza kuuzwa kuanzia mwanzo wa mwaka 2015.
Itakuwa aina mpya ya bidhaa yenye lengo la kufanya kazi na vifaa vingi zaidi vya mawasiliano kuliko kompyuta nyingine za kawaida.
Kwa hiyo kuanzia Septembe 30 hadi mwaka 2015, watu wataweza kupata matoleo ya majaribio kwa ajili ya shughuli hizo hizo za majaribio ili kurekebisha, kuandika na kuangalia chochote ambacho kimekosewa .
Kuna mabadiliko kadhaa yanatarajiwa kuwamo kwenye windows 10 ili kuweza kushika soko la watumiaji wa kompyuta na vifaa vingine.
Toleo la windows 10 litahusisha muonekano na programu nyingine nyingi zilizokuwapo kwenye windows 7 na windows 8 .
Pia itarejesha kitufe cha ‘start’ ambacho kilipotea kwenye toleo la mwanzo la windows 8 ingawa baadaye kilirejesha kwenye windows 8.1.
Pia inasemekana wataondoa uwezekano wa ‘Touch’ kama zilivyo simu za mikononi kutokana na watumiaji wengi hasa wa windows 7 na xp kupendelea zaidi matumizi ya ‘Mouse.’
Hata hivyo, wataacha iendelee kutumika kwenye vifaa vingine vinavyootumia windows kama simu, ‘touchpads’ na mashine za kutolea fedha.
Kitu kipya ambacho kitakuja kwenye windows 10 ni kwa programu yenyewe kuwa na uwezo wa kujua nini unafanya kwenye kompyuta yako na kuwa na kumbukumbu ya vitu vyote bila hata kutafuta.
Hii itakua ahueni kwa vyombo vya usalama vinavyotafuta taarifa za watu mbalimbali usiku na mchana, lakini pia ni nafuu kwa watu wa matangazo kwa sababu sasa watakuwa na uwezo wa kujua unachofanya na kukupa tangazo hapo hapo kama umejiunga kwenye mtandao .
Kuna suala moja nyeti ambalo Microsoft hawajajibu wala kuongelea, ni tuhuma za kukusanya taarifa kutoka vifaa mbalimbali vya mawasiliano vinavyotumia bidhaa za windows kama simu na kompyuta ambazo zilisababisha Serikali ya China kugoma kuhamia kwenye windows 8 toka windows xp na matoleo mengine ya zamani .
Kama nilivyoandika huko juu, windows 10 inatarajiwa kutumika kwenye vifaa vyote vya mawasiliano, kama ni hivyo tujue tu kama ni taarifa zitakusanywa kutoka kwa watu mbalimbali ambao watajiunga kwenye mitandao kwa ajili ya huduma mbalimbali.
Hivyo, ni suala la taasisi nyingine kujipanga kiulinzi na usalama ili kuhakikisha elimu inatolewa kwa watu kuhusu suala hili .
Mpaka nilipomaliza kuandika makala hii kampuni ya Microsoft haijasema chochote kuhusu gharama au bei za Windows 10.
Pia kuna shaka kama wale wanaotumia windows za zamani watapatiwa huduma bure za kuboresha matoleo hayo kwenda Window mpya.
No comments:
Post a Comment