Tuesday, 11 November 2014

TCRA YAWATAKA WAMILIKI BLOGS KUZITUMIA VIZURI WAKATI WA UCHAGUZI

Mkurugezi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa, John Nkoma akizungumza na  Bloggers (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa leo.


Baadhi ya wamiliki wa Blogs nchini wakifuatilia mkutano huo.
Wadau kutoka  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakifuatilia mada za mkutano wa leo.
Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Injinia Andrew Kisaka akitoa mada katika mkutano na Bloggers leo.
Profesa Nkoma (kushoto) pamoja na Ofisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo, Aron Msigwa (kulia) wakisikiliza maswali kutoka kwa wamiliki wa Blogs (hawapo pichani).
WAMILIKI wa Blogs nchini wametakiwa kuzitumia vyema blog zao katika kuripoti habari na matukio mbalimbali wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, wabunge na urais.
Hayo yamesemwa na Mkurugezi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma leo alipokuwa akizungumza na wamiliki wa Blogs hizo katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Profesa Nkoma alisisitiza kwamba wakati wa uchaguzi wamiliki wa Blogs wanatakiwa kutoa fursa sawa kwa kila upande pasipo upendeleo wowote wala uchochezi.
Aidha katika mkutao huo, wamiliki wa Blogs walikubaliana kuendeleza mchakato wa kuwa na umoja wao uliosajiliwa kisheria ambapo walichagua viongozi wa muda watakaosimamia mchakato huo. 
Uongozi wa muda uliopitishwa na wamiliki hao ni kama ifuatavyo:
1.Joachim Mushi - Mwenyekiti
2. Francis Godwin - Makamu Mwenyekiti
3. Khadija Kalili - Katibu
4. Shamim Mwasha - Mjumbe
5. Othman Maulid - Mjumbe
6. William Malecela 'Lemutuz'- Mjumbe
7.Henry Mdimu - Mjumbe
TCRA imeahidi kutoa ushirikiano katika mchakato huo wa kusajili umoja wa wamiliki wa Blogs na kutoa elimu katika masuala mbalimbali yatakayosaidia jamii.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!