Tuesday, 11 November 2014

NAHODHA JELA KWA AJALI YA MELI KOREA


Ferry hiyo ilikuwa imewabeba wanafunzi waliokuwa katika ziara ya mafunzo

Nahodha wa kivuko cha Korea Kusini ambacho kilizama mwezi Aprili 2014 amepatikana na hatia ya uzembe wa kupindukia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 36 jela.

Kivuko hicho cha Sewol kilikuwa kimebeba watu 476 wakati kilipozama. Zaidi ya watu 300 walikufa, wengi wao wakiwa wanafunzi wa shule.
Lee Joon-seok alikuwa miongoni mwa wafanyakazi wa meli 15 wanaokabiliwa na mashitaka kufuatia kuzama kwa meli hiyo, katika ajali mbaya kuliko zote kuwahi kutokea nchini Korea Kusini.
Waendesha mashitaka walimshtaki kwa Lee kwa makosa ya kuua pasipo kukusudia na kutaka apewe adhabu ya kunyongwa hadi kufa, lakini majaji wameiondoa adhabu hiyo.
Lee ambaye yuko katika umri wa mwisho wa miaka 60, na adhabu aliyopewa ya kifungo jela, ni wazi kwamba atakuwa amefungwa kifungo cha maisha, anasema mwandishi wa BBC, Steve Evans kutoka mjini Gwangju.
Swali kuu katika kesi hii lilikuwa kama kulikuwa na dhamira ya kuua na kulikuwa na ushahidi wa uzembe.
Katika tukio la kuzama kwa meli Lee ambaye alikuwa nahodha wa meli hiyo alionekana kuondoka katika meli hiyo iliyokuwa ikizama wakati abiria wengi wangali bado ndani ya meli hiyo.
Wakati wote wa kesi hiyo, Lee aliomba msamaha kwa kuwatelekeza abiria wake.

Bwana Lee amapetikana na hatia ya uzembe kupindukia

Wafanyakazi wengine 14 wamefungwa kutokana na makosa mbalimbali.
Mhandisi mkuu wa kivuko hicho, ambaye alitambuliwa kwa jina la ukoo la Park, alipatikana na hatia ya mauaji na kufungwa miaka 30 jela.
Wafanyakazi wengine 13 walipewa vifungo vya kufikia miaka 20 kwa makosa ya kuwatelekeza abiria na kukiuka sheria za bahari.
Ndugu wa washitakiwa walifadhaishwa na hukumu hiyo, huku baadhi wakilia.
Mwanamke mmoja ameripotiwa kupiga mayowe katika chumba cha mahakama: "Si haki. Je nini kinafanyika juu ya maisha ya watoto wetu? Watuhumiwa wanastahili adhabu mbaya zaidi ya kifo."
Ajali hiyo ilisababisha huzuni nchini kote, na kuwepo malalamiko ya usimamizi mbaya wa vivuko na mamlaka zinazohusika na uzembe katika kukabiliana na dharura.
Saa chache kabla ya kutolewa hukumu, serikali ya Korea Kusini walisitisha utafutaji wa miili katika kivuko hicho, ambayo ilizama tarehe 16 Aprili.
Miili 295 iliweza kunasuliwa kutoka meli hiyo na wazamiaji lakini tisa hawajulikani walipo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!