Saturday 15 November 2014

NABII ALIYEJITABIRIA KIFO AFARIKI DUNIA

Dar es Salaam. Mwanzilishi wa Kanisa la The Pool of Siloam, Nabii Eliya Adam amefariki dunia juzi mchana, muda mfupi baada ya kuwaeleza wasaidizi wake kuwa siku hiyo ndiyo ilikuwa ya mwisho kwake kuishi duniani.

Nabii huyo ilianzisha kanisa hilo mwaka 2003 katika eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam, baadaye kuenea mikoa mbalimbali nchini.
Akitoa taarifa za kifo cha Nabii Eliya, Kuhani kiongozi wa kanisa hilo, Miaka 1000 Eliya alisema kabla ya kifo chake, Nabii aliwaita na kuwaeleza mambo manne.
“Kwanza, alituambia amemaliza kazi ya kulijenga kanisa, pili akasema gari lake lipo tayari na litakuja kumchukua leo mchana (juzi mchana). Baada ya kufariki ndiyo tukajua kwamba alipotueleza gari linakuja kumfuata kumbe ni kifo,” alisema.
Alisema nabii pia aliwataka kuhakikisha wanajenga makanisa ya kutosha na kuwataka waumini wa kanisa hilo kukamilisha kila jambo walilopanga.
Alisema Nabii Eliya alikuwa na umri wa miaka 54 na ameacha mke na watoto wanne. Mazishi yatafanyika Jumapili.





UTATA WAFUNIKA KIFO CHA NABII ELIYA. ALIKUWA NI MWANZILISHI WA KANISA LA SILOAM, SHIKA NENO TENDA NENO


Kuanzia jana kumekuwa na post kutoka kwa watu tofauti tofauti katika mitandao ya kijamii kutokana na kifo cha aliyekuwa mwanzilishi wa kanisa la siloam nabii Eliya. moja ya post ni hapo chini. Kuna habari zinaenea kwa kasi katika mitando ya kijamii ya kwamba ,mwenye mafundisho tata ,Ndungu Munuo,aka Adamu wa Pili, Nabii Eliya, Bwana wa Majeshi, Mjumbe wa Mapenzi ya Mungu wa Kizazi cha Nne, Amefariki Dunia jana usiku, Mpaka sasa hakuna tangazo rasmi la Kanisa la Siloam. Sitofahamu hiyo inatokana na kutokuwa na taarifa za uwazi za kifo chake.

 kutokana na sintofahamu hiyo blog hii ilifanya mawasiliano na mmoja wa washirika wake kutaka kujua uharisia wa jambo hilo Kwa mujibu ya Mshirika niliyeongea nae amesema kuwa nabii Elia amelala na wala 
hajafa na hakuna kulia maana aliwaaga watu wote wakiwamo ndugu zake na familia yote na jambo hili lilikuwa linajulikana kuwa atalala na alishatafuta hadi mrithi wake ambaye ataendeleza kazi. anategemewa kulazwa mlima wa
moto (nyumbani kwake) mbezi bichi siku ya tano ya umbaji ambayo ni j2. aliongeza kusema kuwa muda wa yeye kutumika wa miaka 3 ulishaisha hivyo alishamaliza kazi.

 alinipa mifano kuwa manabii wengi walifanya kazi kwa miaka 3 na wakawa wamemaliza kazi yao hivyo na nabii Elia kuanzia ameanza kazi miaka 3 ilishafika ni lazima aondoke ili wengine waendelee. Mshirika huyo alikuwa anaongea kwa ujasiri na kujiamini kana kwamba alishafundishwa namna ya kujibu, kutokana na mahojiano niliyofanya nae ni kweli Nabii Eliya kafariki na maandalizi ya kumlaza nyumbani kwake zinaendelea haijafahamika kama alikuwa anaumwa au alifariki ghafla. 

Aliyekuwa Nabii Eliya wa kanisa la siloam shika neno trnda neno Nabii Eliya akiwa madhabahuni Wafuasi wakijipanga wakati wa yeye kuingia Kwa heri nabii Eliya

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!