Mwalimu mstaafu wa Shule ya Msingi Vikonge Wilayani hapa Rashiid Mbogo(62) Mkazi wa Kijiji cha Majalila Kata ya Mpanda Ndogo Wilaya ya Mpanda amefikishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa maika mitano
Mtuhumiwa alifikishwa kizimbani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa na kusomewa mashitaka na mwendesha mashitaka Mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi Naathaniel Silomba
Mwendesha mashitaka alidai mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo hapo Oktoba 19 mwaka huu majira ya saa mbili usiku huku akiwa nyumbani kwake
Mtuhumiwa anadaiwa siku hiyo ya tukio alikuwa amekaa sabuleni akiwa akisubiria chakula cha usiku kilichokuwa kikiandaliwa jikoni na bibi ya mtoto huyo ambae ni mke wa mtuhumiwa
Mwendesha mashitaka aliiambia mahakama wakati akiwa anaendelea kusubilia chakula mtuhumiwa alimwita mjuu kuu wake sebuleni na kisha alimweka juu ya mapaja yake na alivua nguo na kuanza kumbaka huku mtoto huyo akiwa anapiga kelele za kuomba msaada
Mwendesha mashita Silomba aliendelea kuieleza mahakama kuwa baada ya kusikia mayowe ya mtoto huyo Bibi wa mtoto na majirani waliingia ndani ya nyumba sebuleni na kukuta mtoto huyo huku akiwa anatokwa na damu nyingi kwenye sehemu zake za siri na huku akiwa analia kutokana n maumivu makali aliyokuwa ameyapata
Baada ya kusomewa mashitaka hayo mtuhumiwa alikana mashitaka hayo ambayo alikuwa amesomewa na mwendesha mashitaka
Hakimu Chiganga aliieleza mahakamani kuwa mdhamana wa mshitakiwa uko wazi kwa ajiri ya mdhamana endapo mshitakiwa atamiza mashariti ya mdhamana
Ambapo mshitakiwa alitakiwa awe na mdhamini mmoja mwenye mali isiyohamishika yenye thamani ya shilingi milioni tano hata hivyo mshitakiwa alishindwa kutimiza masharti ya mdhamana
Mtuhumiwa alipelekwa rumande ambapo Hakimu Chiganga aliihairisha kesi hiyo hadi hapo Novemba sita itakapo tajwa tena
Yapo makosa ambayo ni makubwa kama vile wizi wa kutumia silaha , unyang’anyi na kupatikana na dawa za kulevya adhabu zake ni k ndogo kuliko adhabu ya kosa la ubakaji lakini hayana dhamana huku kosa la ubakaji lenye adhabu kubwa dhamana yake inakuwa ikowazi
Na Walter Mguluchuma
Katavi
No comments:
Post a Comment