Thursday 13 November 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AKABIDHI TUNZO KWA WASANII BORA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimkabidhi tunzo ya Msanii bora katika masuala ya kijamii (HUMANITARIAN AWARD) Bw. Patrick Kungalo kwa niaba ya Fr. Canute Mzuanda kwenye hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 13,2014 Ikulu Dar es salaam. Makamu wa Rais alikutana na jopo la waandaaji wa siku ya Msanii, Kampuni ya Haak Neel Production, Baraza la Sanaa la Taifa na Wizara ya Habari, Vijana Michezo na Utamaduni na kutoa zawadi ya fedha shilingi milioni kumi ambazo aliahidi siku kilele cha siku ya Msanii Tanzania iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Oktoba 25,2014
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati akiwa katika picha ya  pamoja na washindi wa tunzo ya msanii bora na Viongozi wa Wizara ya Habari baada ya kukabidhi tunzo hizo katika hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 13,2014 Ikulu Dar es salaam.               (Picha na OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati akiwa katika picha pamoja na washindi wa tunzo ya msanii bora baada ya kuwakabidhi tunzo hizo kwenye hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 13,2014 Ikulu Dar es salaam.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!