Monday 17 November 2014

MAANDAMANO YAFANYIKA KENYA KUPINGA KITENDO CHA MWANAMKE KUVULIWA NGUO KWA MADAI YA KUVAA NGUO FUPI

Maandamano hayo yamefanyika chini ya kauli mbiu 'My dress my choice'

Wanawake mjini Nairobi, Kenya leo wameandamana kupinga kitendo cha mwanamke mmoja kuvuliwa nguo wiki jana kwa madai kuwa
alikuwa amevalia sketi fupi sana.

Wanawake wengi walikerwa na kitendo hicho wakisema kuwa kila mwanamke ana haki ya kuvalia mavazi yanayomfurahisha.
Hiyo wiki jana kanda ya video ilisambazwa kwa mitandao ya kijamii ikionyesha mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina hadi sasa akivuliwa nguo zake na wanaume katika kituo cha magari ya abiria kati kati mwa Nairobi.
Wanawake mashuhuri wakiwemo wasanii, wanasiasa na wanaharakati walilaani kitendo hicho wakihoji kwani mavazi ya mwanamke yanamhusu nini mwanamume ambaye sio mumewe wala jamaa yake.
Baadhi walikitaja kitendo hicho kuwa cha kinyama na kinachokiuka haki za wanawake.
Msanii mmoja mashuhuri Nyota Ndogo alinukuliwa akisema ikiwa wanaume wanawavua nguo wanawake kwa kile wanachosema ni mavazi yasiyo ya kiheshima, basi na wanaume wanaolegeza long'i zao na wao basi pia wavuliwe nguzo zao.
NIONAVYO MIMI NA TANZANIA PIA MAANDAMANO HAYA YAFANYIKE WANAWAKE WANANYANYASIKA KISA MTU KAVAA NGUO FUPI, SASA IMEKUWA TOO MUCH" WATU WANAVULIWA NGUO BARABARANI KAMA SI UNYANYASAJI NI NINI? KAMA NI MAADILI NA WAO WAMEKOSA MAADILI KWA KUMDHALILISHA MWANAMKE! NACHUKIA SANA !


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!