Monday, 17 November 2014
JINSI VVU VINAVYOSTAWI MWILINI
Mwanzoni mwa miaka ya 80 ni mambo machache sana yalofahamika kuhusu ukimwi'upungufu wa kinga mwilini'ukimwi.Madaktari walifahamu kwamba uliathiri mfumo wa kinga na kwambamboti haukuwa ugonjwa wa kinasaba au wa kurithi bali mtu angeweza kuupata toka kwa mwingine aloambukizwa.
Mwaka wa 1984 wanasayansi waligundua chanzo cha ukimwi ni kirusi Human immuno-deficiency virus'HIV'au Virusi Vya Ukimwi'VVU'ambao umewezesha madaktari kukuza ufahamu mzuri sana wa ugonjwa,namna kirusi kinanavyoambukizwa kutoka mtu moja mpaka mwingine,mzunguko wa maisha ya kirusi kinavyostawi na kuathiri afya ya mtu aloambukizwa.Karibu asilimia 50 ya wote wenye VVU wanaambukizwa kabla ya kufikisha miaka 25 na Ukimwi ndio sababu ya pili inayojulikana kwa wenye umri wa miaka 20-35.VVU huishi na hustawi popote mwilini penye majimaji,huonekana tu kwa hadudubini,haina umbile la msingi na ndo maana yahitaji seli mwenyeji kujidurufu chenyewe.Kitiba VVU vimeainishwa kama Lentivirus ambayo ni jamii ya virusi vya retrovirus.VVU vimebobea ktka kushambulia seli ya T4 kwa sababu seli hizo zina molecule kipokzi inayoitwa CD4 ambapo kwenye utando wake VVU hujifunga vizuri na ili kujizalisha chenyewe kirusi kinaanzisha ktka seli kinasaba ambazo zitalazimisha seli mwenyej kufanya nakala ya virusi na kwa kufanya hivyo VVU huua seli mwenyeji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment