Wednesday 19 November 2014

HABARI KAMILI KUHUSU MTOTO ALIYUAWA KINYAMA HUKO MAJOHE JIJI DAR--ES-SALAAM

WIMBI la utekaji na mauaji ya watoto katika Jiji la Dar bado ni tishio kufuatia wiki iliyopita, maiti ya mtoto Nuru Mohamed (7) mkazi wa Majohe Kichangani Wilaya ya Ilala, kuokotwa ikiwa imeharibika vibaya, tena baadhi ya viungo vyake vikiwa vimenyofolewa.
Mtoto Nuru Mohamed (7) aliyetekwa na kuuawa na mtu asiyefahamika.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Novemba 6, mwaka huu, majira ya saa 12 jioni, baada ya watoto wenzake aliokuwa akicheza nao kudai kuwa Nuru alichukuliwa na mtu aliyekuwa amevalia mavazi ya Kininja na kutokomea naye.


Mama wa mtoto Nuru akiwa naye enzi za uhai wake.
Baadhi ya mashuhuda waliokuwa eneo la tukio, walisema mwili wa mtoto huyo ulikutwa ukiwa hauna sehemu za siri, matiti, nyama ya kisogoni na makalio kukatwa na kuzibwa na gundi hali iliyoashiria ushirikina.
Masheikh wakiuswalia mwili wa mtoto Nuru.
BABA MZAZI PICHANI ASIMULIA ILIVYOKUWA
“Nakumbuka siku ya kutoweka kwake, nilikua kazini nikapigiwa simu saa 12.45 jioni na kuelezwa Nuru ametekwa na mtu aliyevaa kininja, aliyemrubuni kwenda kumnunulia biskuti. “Nilielezwa kwamba muda mfupi baada ya kutoweka, watoto wenzake walipatwa na hofu na kumwambia mama yake kwamba kuna mtu kaondoka na marehemu hali iliyomfanya kuinuka na kuanza kufuatilia bila mafanikio.
Majirani wakimfariji mama wa mtoto Nuru.
“Niliungana na mke wangu pamoja na ndugu wengine kumtafuta hadi asubuhi bila mafanikio, nikiwa nipo maeneo ya Chamazi saa 2 asubuhi nilipigiwa simu na kuambiwa mwili wa mwanangu umepatikana maeneo ya lwa Mkandawile ukiwa umeharibika, nilienda na kukuta kuwa ni yeye.
Waombolezaji wakiwa katika msiba wa marehemu Nuru.
“Tulitoa taarifa polisi ambao walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili hadi Hospitali ya Amana na muda mfupi baada ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari tuliuchukua na kuuzika makaburi yaliyopo maeneo ya ninakoishi,” alisema.
Mjunbe wa Shina namba 15 Tawi la Majohe, Matanzira Thomas maarufu kwa jina la Kobra akiwa ofisini.
Mjunbe wa Shina namba 15 Tawi la Majohe, Matanzira Thomas maarufu kwa jina la Kobra alisema kwamba matukio hayo ya utekaji watoto, kuwaua na kuondoka na sehemu ya viungo ni hatari hasa katika nchi ya amani kama Tanzania, hivyo ameliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini na kuwakamata watu hao hatari.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!