Sunday 16 November 2014

FRIENDS RANGERS WANASHUKA KATIKA UWANJA WA KARUME LEO

images
Mwandishi Wetu
VINARA wa Ligi Daraja la kwanza katika kundi A, timu ya
Friends Rangers, leo wanashuka katika Uwanja wa Karume,
Dar es Salaam, kuvaana na timu ya Kimondo, katika mchezo
wa Ligi Daraja la Kwanza.

Ofisa Habari wa klabu hiyo,
Asha Kigundula, amewataka wapenzi wa klabu hiyo kujitokeza
kwa wingi katika mchezo huo, kuwapa hamasa wachezaji wao.
Kigundula alisema kuwa wana amini mchezo huo utakuwa
mgumu, lakini kujitokeza kwa wapenzi wengi kutawafanya
wachezaji wao wawe na hamasa kubwa na kuweza kupata
ushindi katika mchezo huo.
Alisema kuwa kikosi chao tayari kipo kambini kujiandaa na
mchezo huo, ambao ni muhimu kushinda, ili kiweze kupigania
nafasi ya kupanda Ligi Kuu msimu ujao.
Kigundula alisema kuwa kushinda kwao katika mchezo wao
uliopita dhidi ya Majimaji, kumeisaidia timu yao kuzidi kupaa na
kukaa juu ya msimamo wa kundi lao.
Alisema kushinda kwao katika mchezo huo ni juhudi binafsi za
wachezaji, viongozi na wapenzi wa timu hiyo kwa sababu
walikuwepo na kuwapa ushirikiano mwanzo.
Katika mchezo wa huo uliyofanyika kwenye Uwanja wa
Karume, Dar es Salaam, Friends Rangers iliwapa kichapo cha
mabao 2-1 timu ya Majimaji ya Songea.
Kwa matokeo hayo Friends Rangers wanaongoza kundi kwa
pointi 19 huku maji maji ambao ndio walikuwa wakiongoza ligi
hiyo katika kundi hilo wakishushwa na kubakia na pointi zao 18.
VIA-FULLSHANGWE

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!