Tuesday, 4 November 2014
EDEM KODJO KUMALIZA MGOGORO BURKINA FASO
Umoja wa Afrika umemteua waziri mkuu wa zamani wa Togo kuwa mjumbe maalum wa Burkina Faso kufuatia maandamano ya hivi karibuni yaliyomuondoa madarakani Blaise Compaoré,
Rais Blaise Compaoré aliyejiuzulu. TUME ya Umoja wa Africa siku ya jumatatu imemchagua Edem Kodjo kutoka kambi ya Pan Africa kama mjumbe wa Burkinafaso baada ya baraza la amani na usalama kutoa wiki mbili za kurejesha wananchi kuwa katika hali ya kawaida Uteuzi wa Kodjo ni sehemu ya juhudi za umoja wa Afrika kutafuta njia za usuluhishi kufuatia mgogoro unaoikabili nchi ya Burkinafso Kodjo Atafanya kazi ya kusaidia kuanzishwa kwa utawala wa kiraia kwa njia ya demokrasia katika kipindi cha mpito hadi katika tarehe za uchaguzi Hata hivyo jeshi la nchi hiyo lilichukua madaraka ya kuongoza nchi hiyo baada ya ya shinikizo la kujiuzulu kwa rais Compaore wiki iliyopita aliyetaka kuongeza muda wa utawala wake.
Kodjo, ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu wa Togo manamo mwaka 1994 na 1996, pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Afrika (OAU) ambayo kwa sasa katika kipindi cha mwaka 1978 hadi 1983.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment