Saturday 1 November 2014

DK. DAU ASHAURI TIBA YA MSONGAMANO DAR


MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk Ramadhani Dau amesema njia ya kupunguza msongamano katika jiji la Dar es Salaam ni kuzuia malori kuingia mjini kwa kujenga bandari kavu nje ya mji, akisema hilo likifanikiwa, msongamano unaweza kupungua kwa asilimia 40.


Akizungumza juzi mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alipotakiwa kueleza maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Dau alisema miaka mitano baada ya kukamilika kwa daraja hilo litaonekana kutosaidia chochote kutokana na mipango ya maendeleo inayofanywa Kigamboni.
“Mizigo ikifika bandarini inaweza kusafirishwa hadi nje ya mji kwa njia ya reli na baada ya hapo kubebwa na malori, na hata hili la kila baada ya nyumba moja kuwa na yadi ya magari linaweza kuondolewa kwa kujenga nje ya mji, hii itapunguza msongamano kwa asilimia 40,” alisema.
Alisema NSSF imejipanga kujenga bandari kavu kati ya kijiji cha Vihingo, Kisarawe, Soga, Chalinze au Kibaha katika kupunguza foleni na kupunguza makontena katika Bandari ya Dar es Salaam.
Kuhusiana na ujenzi wa Daraja la Kigamboni na barabara za maungio inaendelea vizuri na kuwa umefikia asilimia 69 na utakamilika mwezi Julai, 2015.
Kwa kiasi kikubwa, jiji la Dar es Salaam limekuwa na msongamano mkubwa wa magari ambao kwa kiasi kikubwa unatajwa kuchangiwa na malori yanayoingia na kutoka bandarini.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!