Ripoti kutoka kaskazini mashariki mwa Nigeria zinasema kuwa wanamgambo wa Boko Haram wameudhibiti mji wa Chibok , mji ambapo waliwateka nyara zaidi ya wasichana 200 mwezi Aprili.
Wenyeji walisema kuwa wanamgambo hao walivamia mji huo siku ya alhamisi na hadi sasa mji huo uko chini ya udhibiti wao.Seneta mmoja kutoka eno hilo ameiambia BBC kuwa wanajeshi waliokuwa wakiulinda mji huo walitoroka wakati wanamgambo hao walipofanya uvamizi.
Boko Haram wamekuwa wakiendesha uvamizi kwenye sehemu zilizo karibu na Chibok mara kadhaa tangu wawateke nyara wasichana wengi kutoka shule moja eneo hilo.Tangu wakati huo watu wamekuwa wakilalamika kuwa eneo hilo halijapewa ulinzi wa kutosha.
(Stori: BBC
No comments:
Post a Comment