Monday, 10 November 2014

BILIONEA DANGOTE AVUTIWA NA KIWANDA CHAKE CHA MTWARA


MFANYABIASHARA namba moja kwa utajiri Afrika, Alhaji Aliko Dangote, amevutiwa na kasi ya ujenzi wa kiwanda chake cha saruji, kinachojengwa mkoani Mtwara.



Alisema kutokana na kasi hiyo, anaamini ujenzi utakamilika kwa muda muafaka, na uzalishaji wa saruji kuanza Juni mwakani kama walivyopanga.
Akizungumza mkoani hapa juzi baada ya kupata maelezo ya ujenzi kutoka kwa uongozi wa Kampuni ya Sinoma ya China inayojenga kiwanda hicho, na kuangalia namna ujenzi unavyoendelea, Dangote alisema ameridhika na hatua iliyofikiwa.
“Nina furaha maendeleo ya ujenzi ni mazuri, wanajenga kwa kasi kubwa, naamini tutafikia malengo yetu ya kuanza uzalishaji ya saruji Juni mwakani,” alisema Alhaji Dangote.
Pia, alisema kuwa kiwanda hicho kitaanza uzalishaji wake kwa kutumia makaa ya mawe na watatumia nishati ya gesi, itakapoanza rasmi kuzalishwa.
“Tutaanza kuzalisha kwa kutumia makaa ya mawe, hatujajua gesi itakuwa inauzwa kwa shilingi ngapi kwa uniti moja ila ni vizuri pia kutumia nishati ya gesi,” alisema.
Kwa mujibu wa makubaliano, mradi huo unatakiwa kukabidhiwa Juni 2015, na kuanza uzalishaji, lakini kampuni ya Sinoma iliyopewa jukumu ya ujenzi wa mradi huo, imeeleza kuwa watakamilisha ujenzi Aprili mwakani.

HABARI LEO.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!