Thursday, 20 November 2014
AINA ZA PUMU'ASTHMA'
Pumu ni hali inayomfika mtu anaposhindwa kupumua kwa njia ya asili.
CHANZO:-Athari za kinasaba'Genetical disorders'-Uvutaji sigara kipindi cha ujauzito-Magonjwa ya
mapafu'Bronchitis'-Mzio'Allergies'kama vumbi,vinyesi ya wanyama,baadhi ya
vyakula,uchafuzi wa mazingira kama moshi na harufu kali-Baadhi ya kemikali maeneo ya
kazi haswa viwandani kama vya rangi,chuma,sementi na vigae-Matumizi ya dawa za
kushusha shinikizo la damu jamii ya beta blockerss kama vile prapanolol-Magonjwa kwenye mfumo wa kupumua yasababishwayo na virusi/bakteria kama rhinovirus,chlmydia pneumonia au bordeletella pertusis-Matumizi ya mapema sana ya dawa hasa antibiotic kwa watoto hubadili mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na hivyo kumfanya mtoto kuwa ktka hatari ya kupata pumu-Msongo wa mawazo husababisha pumu na matatizo ktka mfumo wa upumuaji-Upasuaji wakati wa kujifungua'Caesarian section'-Magonjwa ya ngozi'Eczema'-Homa ya vumbi'Hay fever'.AINA ZA PUMU:
1-Pumu hatari isobadilika'Status Asthmaticus'pamoja na matumizi ya vitanua njia ya hewa'Broncholidators'na vipoza mcharuko'Steroids'mgonjwa wa aina hii ya pumu anaweza asipate nafuu ya haraka na kupoteza maisha.2-Pumu kwa wanaofanya mazoezi kupita kiasi'Exercise induced Asthma'Wakati wa mazoezi mtu hupumua kutumia pua na kupitia mdomo hata hivyo wakati wa mwingine hutokea hewa aivutayo huingia ndani bila ikiwa haijapoozwa vya kutosha puani na kusababisha ongezeko la mtiriko wa damu ktka mishipa inayosambaza damu ktka mirija ya kupitisha hewa na kusababisha kuvimba kwa kutaka za mirija hiyo na mhusika kupata shambulizi ya pumu.3-Pumu itokanayo na kazi uifanyayo'Occupational induced Asthma'Mazingira ya kazi kama anayeshinda na feni/ac,anayeendesha gari,anayetengeza vigae,matairi,matofali,rangi,kemikali,mbolea,chuma,unga na mbao nk.
DALILI:--kubanwa kifua,kushindwa kupumua na kutoa sauti ya miruzi'wheezing sound'.USHAURI-ni vema uwahi kwa daktari uonapo dalili tajwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment