Friday 10 October 2014

WAHAMIAJI 26 WAKAMATWA TABORA


WAHAMIAJI 26 kutoka nchi jirani za Burundi na Rwanda wamekamatwa juzi katika Kijiji cha Mlogolo, kilichopo Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora ambao kati yao, 22 ni watoto wenye umri chini miaka 15.

Akizungumzia tukio hilo,Ofisa Uhamiaji mkoani humo,Andrew Kalengo, alisema wahamiaji hao walikuwa wakisafirishwa kwenda katika Wilaya ya Chunya,mkoani Mbeya ili kutumikishwa katika mashamba ya tumbaku.
"Hawa wa hamiaji walikuwa wakisafirishwa kwa lori wakitokea
Mkoa wa Kigoma uliopokatika mpaka wa Tanzania na Burundi, hivi karibuni vitendo vya kusafirisha wahamiaji vinaongezeka kwa kasi katika mikoa mingi ukiwemo Tabora jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa nchi," alisema.
Alisema idara yake imejipanga kupambana navitendo hivyo kwa kuongeza doria ili kuwabaini wahamiaji haramu ambao wanatumikishwa na wanaoishi nchini kinyume cha sheria kutoka nchi jirani za Burundi na Rwanda.
"Kuna kikundi chawatu wachache kinachofanya biashara yakuwasafir isha maeneo mbalimbali nchini ilikuwauza kwa watu wanaohitaji vibaruawa kutumikisha katika shughuli zao hususan kilimo cha tumbaku,"aliongeza.
Watoto waliokamatwa Prosper John na Sifa Gwagaza ambao ni raia wa Burundi na Buyoya Lezeri, raia wa Rwanda,walisema hawakujua wanapelekwa wapi na kufanya nini.
"Tulishawishiwa kujaTanzania na kuambiwa kuna kazi nzuri za kufanya...tunaomba kurejeshwa nyumbani,"walisema .
Baadhi yawakazi wa Mkoa huo,wameishauri idara hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi,kuwasaka na kuwakamata watu wanaojihusisha na biashara hiyo.
Mtuhumiwa anayedaiwa kufanya biashara ya kuuza watoto,Bw. Robson Mwendo,alidai hafanyi biashara ya binadamu bali aliwachukua ili kwenda kuwaajiri katika mashamba yake .
Dereva wa lori lililobeba wahamiaji hao,Seleman Kagambo, alisema aliwabeba kama abiria hakujua kama ni wahamiaji.


CHANZO: Majira

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!