Friday 10 October 2014

DUNIA YALAUMIWA KWA KUTODHIBITI EBOLA

Shirika la madaktari wasio na mipaka wanaotoa huduma za kitabibu nchini za Afrika Magharibi dhidi ya Ebola limesema dunia inapaswa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na janga la ugonjwa huo.

Rais wa chama cha madaktari wasio na mipaka Medecins sans Frontieres Joanne Liu amesema anashindwa kuelewa kwamba ni kwanini ikiwa ni miezi saba sasa tangu kulipuka kwa ugonjwa huo hadi ambapo hakuna hatua za haraka za kidunia zilizochukuliwa hadi sana.
Amelinganisha hatua za kimataifa zilizochukuliwa wakati wa janga la tetemeko la ardhi la Haiti mwaka 2010 kwamba makundi ya misaada ya kibinadamu yalikusanyika katika eneo hilo kwa lengo la kutoa misaada ndani ya saa 48 tu sasa iweje katika janga hilo ambalo limeshachukua muda mrefu.
Rais Joanne amsema idadi ya watalaam 300 waliowasili Liberia kutoka Marekani ni ndogo hali ambayo inaonyesha wazi kuhitaji kwa wataalamu zaidi.
BBC.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!