Sunday, 7 September 2014

WAZIRI MWAKYEMBE ATEMBELEA ENEO LA AJALI YA MABASI MUSOMA, AWAJULIA HALI MAJERUHI

Waziri wa Uchukuzi, Dkt Haririson Mwakyembe akiwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani, Mohamed Mpinga, wakiangalia gari la Mwanza Coach walipotembelea eneoe la ajali jana.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, ACP Philipo Kalangi kulia, akiwa na Dkt Harrison Mwakyembe, wakiangalia gari dogo aina ya Nissan Terano linalodaiwa kupata ajali baada ya kugongwa na basi la Mwanza Coach na kutumbukia mtoni.

Dkt Mwakyembe, Waziri Gaudensia Kabaka na Dkt Samson Winani (mwenye shati la kitenge) wakimwangalia mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akimjulia hali Mwandishi wa Habari wa Raia Tanzania, Veronica Mwakyembe ambaye alikuwa amelezwa Musoma.
Mawaziri Dkt Harison Mwakyembe na Gaudensia Kabaka walifurahia jambo wakati wakimjulia hali Frorance Focus.
Meya wa Manispaa ya Musoma, Kisurura akimpa pole Kenneth Chilemile mkazi wa Nyegezi Mwanza, aliypata ajali akiwa katika gari dogo aina ya Nissan Terano, ambapo baba yake Ibrahimu Mashida pamoja na dereva wake walipoteza maisha.
Wahudumu wa afya wakisaidiana kusukuma kitanda cha mgonjwa wa ajali ya Mwanza Coach na J4 Express.
Mwandishi wa Mwananchi, Florance Focus akiwa amelazwa katika Hopitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara baada ya kupata majeraha kichwani na miguuni. Hata hivyo amehamishiwa Bugando kutokana na hali yake kuwa mbaya.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma, Ahmed Sawa na Meya wa Manispaa ya Musoma, Kisurura wa kwanza kushoto wakimjulia hali Mwandishi wa Mwanacnhi Florance Focus baada ya kupata ajali.
Mwandishi wa Channel Ten, Augustine Mgendi akimwangalia Veronica Mwakyembe aliyepata ajali akisafiri na basi la Mwanza Coach. Mwakyembe ambaye ni mwandishi wa habari wa Raia Tanzania amehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kutokana na kupata mvunjiko kwenye bega na majeraha ya mguu wa kushoto.
Waombolezaji wakiwa wamebeba majeneza ya miili ya marehemu waliokufa katika ajali ya mabasi ya Mwanza Coach na J4 Express wakienda kuzika katika makaburi ya Musoma.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!