Wednesday 3 September 2014

WAWILI WAACHIWA HURU KESI YA MAUAJI UBUNGO

index

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewaachia huru washtakiwa wawili katika kesi ya mauaji ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wa mkoani Morogoro na mfanyakazi wa Benki ya NMB, maarufu kama mauaji ya Ubungo Mataa.




Wakati washtakiwa hao wakiachiwa huru, wengine 14 katika kesi hiyo walipatikana na kesi ya kujibu, hivyo watapanda kizimbani kujitetea.

Walioachiwa huru ni mshtakiwa wa sita, Jackson Issawangu na Mussa Mustafa aliyekuwa mshtakiwa wa 10. Mahakama iliridhika na maelezo ya awali na kuwaona washtakiwa hawana kesi ya kujibu.

Issawangu na Mustafa na wengine 14, walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya, D 6866 Konstebo Abdallah Marwa na mfanyakazi wa NMB tawi la Wami Morogoro, Ernest Manyonyi.

Konstebo Marwa na Manyonyi waliuawa Aprili 20, 2006, saa 6 mchana, eneo la Ubungo Mataa jijini Dar es Salaam kwenye makutano ya Barabara ya Morogoro na Sam Nujoma katika tukio la uporaji wa fedha mali ya NMB.

Walikuwa wakisafirisha fedha hizo kutoka Dar es Salaam kwenda Tawi hilo la NMB Wami Morogoro. Sh150 milioni ziliporwa katika tukio hilo.

Katika uamuzi wa mahakama uliotolewa na Jaji Projest Rugazia anayesikiliza kesi hiyo, aliawaachia huru akisema kuwa hakuna ushahidi unaowagusa na kuwahusisha na mashtaka hayo.

Hadi wanaachiwa huru jana, Issawangu na Mustafa walikuwa wameshakaa rumande zaidi ya miaka minane

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!