WAKAZI wa Butimba, Wilaya ya Nyamagana
jijini hapa wanahofia kulishwa nyama ya mbwa
kufuatia ngozi za mnyama huyo kuokotwa
mara kwa mara zikiwa zimechunwa na
kuondolewa kwato .
jijini hapa wanahofia kulishwa nyama ya mbwa
kufuatia ngozi za mnyama huyo kuokotwa
mara kwa mara zikiwa zimechunwa na
kuondolewa kwato .
Hivi karibuni, ngozi nyingine ya mbwa
iligundulika saa 5: 00 asubuhi eneo la kona ya
kuelekea Gereza Kuu la Butimba ambapo
wananchi wa eneo hilo walikusanyika
kuishuhudia .
Hata hivyo , haikuweza kufahamika mara moja
nani anahusika na uchunaji wa ngozi za
mnyama huyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye
eneo la tukio, baadhi ya wananchi walisema
wanahofia kulishwa nyama ya mbwa kwa
muda mrefu bila kutambua.
Walisema kuonekana kwa ngozi hizo za mbwa
mara kwa mara zikiwa zimechunwa ni dalili
kuwa biashara ya uuzwaji wa nyama ya
mnyama huyo inafanyika kwa kificho.
Mmoja watu walioshuhudia ngozi hiyo , Mkushi
Hashim alisema majira ya saa 5: 00 asubuhi
mpita njia mmoja aliiona na kuichukuwa
akidhani ya mbuzi, lakini muda mfupi baadaye
alibaini ni ya mbwa baada ya kugundua
imechunwa kwato.
“ Ilikuwa saa tano asubuhi , kuna jamaa alikuwa
akipita njiani akaichukuwa ngozi hiyo akidhani
ya mbuzi, muda mfupi baadaye akagundua ni
ya mbwa ,” alisema Hashim na kuongeza :
“ Kitendo hiki kinaonesha tunalishwa nyama ya
mbwa kwa muda mrefu bila kugundua kwani
ngozi hiyo alipoileta kijiweni tulithibitisha kuwa
ya mbwa .
“ Ingekuwa kinachookotwa na mwili sawa ,
tungesema ngozi inauzwa mahali kwa ajili ya
urembo au kuwambia ngoma , sasa
kinachookotwa ni ngozi, mwili unakwenda
wapi?”
Mkazi mwingine wa jiji hilo aliyejitambulisha
kwa jina moja la Samwel, alikilaani kitendo
hicho na kusema siyo cha kibinadamu .
Samwel aliongeza kuwa , watu wanaofanya
hivyo ni wauaji na wakitiwa mbaroni
wachukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa
wengine.
“ Tunasikia kuna baadhi ya makabila wanakula
nyama ya mbwa , lakini siyo kufanya hivyo kwa
watu ambao hatuli nyama hiyo , mbaya zaidi ni
kwamba mbwa hao wanaweza kuwa na
magonjwa ya hatari, ” alisema Samwel .
Miaka mitatu iliyopita mkoani Pwani , mtu
mmoja aliwahi kusulubiwa na wananchi
akidaiwa kuwauzia nyama ya mbwa baada ya
kuwalaghai kuwa ni swala.
Mwandishi wetu alifika kwenye ofisi za afya za
mkoa huo kwa lengo la kuzungumza na
wahusika, lakini msemaji hakuwepo ila
mfanyakazi mmoja asiyekuwa msemaji alitoa
rai kwa wananchi kuwa , wajihadhari na ulaji
hovyo wa nyama choma na mishikaki hasa
katika sehemu ambazo si rasmi .
No comments:
Post a Comment