Saturday 27 September 2014

TUTAKUTANA MTAANI" WARIOBA

Warioba: Tutakutana mtaani

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Tume ya Mabadilikoya Katiba, Jaji Joseph Warioba ametabiri kampeni za uchaguzi mkuu ujao kutawaliwa na ajenda ya Katiba mpya ambayo kwa mujibu wake, inaweza kugawa nchi. Jaji Warioba ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu, ameeleza wasiwasi wa rasimu inayopendekezwa kwamba haitapigiwa kura mwaka 2016 badala yake, mchakato wa katiba utaanza upya.


Alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 19 ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Katika maadhimisho hayo yaliyokwenda pamoja na kukumbuka maisha ya aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Marehemu Dk Senkoro Mvungi na kuzindua kitabu chake, Jaji Warioba alisema haupo uhakika wa Katiba mpya kupatikana.
Wasiwasi juu ya upatikanaji wa Katiba mpya unatokana na kile alichosema kwamba haupo uwezekano wa rasimu inayopendekezwa kupigiwa kura mwaka 2016 kutokana na kutokuwepo maridhiano.
Alisema hata katika kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani, suala la Katiba Mpya litakuwa ni ajenda inayoweza kuigawa nchi ikizingatiwa msingi wa kukosekana maridhiano ni aina ya muundo wa Muungano.
“Hakuna maridhiano hasa kuhusu Muungano, rasimu hiyo itaanza kupingwa tangu siku ya kutolewa kwake na wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka kesho Katiba mpya itakuwa ni ajenda inayoweza kuigawa nchi,” alisisitiza na kusema upo uwezekano mkubwa kwamba mwaka 2016 badala ya kupiga kura, mchakato wa kutengeneza katiba ukaanza upya.
Warioba alisema ataendelea kutetea maoni ya wananchi. Alisema wanaotumia vipaza sauti kumuona yeye ni shida, watakutana mtaani ambako kila mmoja akitetea hoja yake, ndipo itakapojulikana shida halisi iliko. Alisema tangu mwanzo matumaini yalikuwa ni nchi kupata Katiba mpya kwa maridhiano.
Alieleza kusikitishwa na mchakato kutekwa na vyama vya siasa kiasi cha maridhiano kutofanywa kipaumbele.
“Kipaumbele ni kupata kura…tangu mchakato huu ulipotekwa na vyama vya siasa, jitihada zilikuwa ni kupata katiba ya makundi, siyo katiba ya maridhiano ya wananchi,” alisema Warioba .
Akosoa rasimu inayopendekezwa Jaji Warioba alikosoa mambo kadhaa yaliyopendekezwa katika rasimu inayopendekezwa, mojawapo ikiwa ni suala la Rais wa Zanzibar kuwa kwenye Baraza la Mawaziri.
Alisema litakuwa jambo tata kwa kuwa yeye (Rais wa Zanzibar) haingiliwi kwa mambo ya Zanzibar.
Alisema lazima patahojiwa haki aliyo nayo kuamua mambo ya Tanzania Bara kwenye Baraza la Mawaziri wakati viongozi wake hawashiriki kuamua mambo ya Zanzibar.
Alisema yeye ni kiongozi wa taifa na atakuwa kwenye Baraza la Mawaziri, lakini hawezi kuwajibishwa wakati Rais, Makamu wa Kwanza na Waziri Mkuu wanaweza kuwajibishwa. Kuhusu madaraka ya wananchi alisema, kwa kuwa katiba inatungwa nao, maoni yao ilikuwa kwamba wawe na madaraka ya kumwondoa mbunge wao kama hawataridhika na uwakilishi wake.
Alisema wananchi pia hawakutaka wabunge kuwa mawaziri ili waweze kuwakilishwa vizuri na ukomo wa ubunge uwe wa vipindi vitatu. Hata hivyo, alikiri kwamba si jambo la kawaida kwa Mbunge kuondolewa madarakani katikati ya kipindi au kuwekewa ukomo, lakini alisisitiza kwamba kwa sababu ya rushwa katika uchaguzi, wananchi wanaona ni vyema watumie madaraka yao kuwawajibisha wawakilishi hao.
“Vyama vya siasa vina madaraka ya kuwaondoa wabunge wao katikati ya kipindi, wananchi nao wanataka watumie madaraka yao,” alisema Warioba akisisitiza Bunge Maalumu liwaeleze wananchi sababu ya maoni yao kuondolewa. Kuhusu mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili alisema pendekezo la kumwondoa rais na mawaziri kutoka kwenye Bunge linakataliwa kwa sababu imezoeleka mfumo wa kibunge kama ilivyo kwa nchi nyingi za Jumuiya ya Madola.
“Siyo kweli kwamba mfumo wetu ni wa kibunge. Kwenye mfumo wa kibunge mkuu wa nchi hana madaraka ya utendaji, madaraka hayo yako mikononi mwa Waziri Mkuu ambaye ni mbunge,” alisema na kutoa mfano wa Uingereza, India, Canada, Australia na hata New Zealand zinazofuata mfumo huo.
Alisema Tanzania ina mfumo wa urais ambao Rais ni Mkuu wa nchi, Mtendaji mkuu na Amiri Jeshi Mkuu.
Alisema Rais na Mawaziri wake kuwa sehemu ya Bunge ni kuchanganya mamlaka na kufanya serikali kuingilia mamlaka ya chombo hicho na pia chenyewe kuingilia mamlaka ya serikali.
Kuhusu tunu za taifa, Warioba alisema Bunge limeondoa uadilifu, uzalendo umoja, uwazi na uwajibikaji kutoka kwenye orodha ya tunu za taifa na kuziweka kwenye misingi ya utawala bora.
Alisema tunu za Taifa ndiyo msingi wa utamaduni na maadili ya taifa, mwelekeo wa taifa utategemea jinsi wananchi wanavyoenzi misingi mikuu na tunu

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!