Tuesday, 9 September 2014

NYANGUMI AONEKANA MTWARA!

WAKAZI wa Msangamkuu, Mtwara Mjini mkoani Mtwara na vitongoji vyake, jana walimiminika katika pwani ya Bahari ya Hindi kumshangaa samaki aina ya Nyangumi mwenye urefu wa futi 48 na tani zaidi ya 30.

Mbali na mshangao huo nyangumi huyo alikuwa kivutio kwa waliomwona huku ikielezwa kwamba mara ya mwisho samaki huyo alionekana zaidi ya miaka 25 iliyopita.
Akizungumza na Tanzania Daima, mvuvi wa samaki huyo Saidi Hassani ‘Ngassa’ alisema Septemba 3 akiwa katika shughuli zake alizivuta nyavu na kubaini kuna uzito usio wa kawaida uliosababisha chombo chake kuvutwa na samaki huyo.
“Baada ya kuona anaweza kuniletea shida nilimuacha samaki huyo akiwa kwenye nyavu nilirudi nyumbani kuwaita watu wengine ili wanisaidie kuvuta nyavu… lakini siku ya kwanza na ya pili ilishindikana hadi siku ya tatu tulimvuta mpaka pwani,” alisema Ngassa.
Ofisa Uvivu Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Saidi Abdallah aliwataka wakazi wa Msangamkuu kutomla samaki huyo kwa kuwa ni sumu, badala yake watumie mafuta yake ambayo ni dawa ya misuli.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!