Tuesday 2 September 2014

MJI WA MBEYA NI KIVUTIO KIKUBWA KWA WATALII...



mlima Rungwe kwa mbali uonekanavyo.


mlima unavyoonekana ukiwa katika mji wa Tukuyu.

ukiwa vijiji jirani karibu na mlima.

Muonekano wa mlima rungwe ambao kwa urefu ni watatu Tanzania ukianza na mlima kilmanjaro  wenye  mita 5,895 ukifuata mlima meru 4,566 na unafuata mlima rungwe  2,960 ambao una, mabwawa yasiyopungua maji wala kuongezeka,  maporomoko ya maji, wanyama mbalimbali wakiwepo na vyula wanaopatikana rungwe tu na nyani aina ya kipunji anayepatikana katika mlima rungwe tu duniani kote. 

Mlima Rungwe ni volkeno iliyozimika ya Tanzania kusini magharibi ikikadiliwa ya kwamba mlipuko wake wa mwisho ulitokea mnamo miaka 2,000 hadi 5,000 iliyopita. mlima huu una kimo cha mita 2,960 ni mlima mkubwa mkoani mbeya. 

Mlima unasimama juu ya ncha kaskazini ya ziwa nyasa, upande wa kusini mashariki wa mlioma hupokea usimbishaji wa milimita 3,000 kwa mwaka ambao ni juu kabisa katika Tanzania.

Mazingira ya mlima ni nchi yenye rutuba na kilimo, pia Rungwe ni eneo la wanyakyusa jina la mlima limekuwa pia jina la Wilaya ya Rungwe 



 Nyumba ya kupumzikia uwapo katika fukwe za ziwa nyasa nyumba hizi huitwa msonge.

Muonekano wa wimbi katika ziwa Nyasa.

 Maji ya ziwa nyasa ni masafi kiasi kwamba unaweza kuona mchanga wake.

Pembezoni kuna safu za milima livingstone iliyosheheni misitu yenye rasilimanyi nyingi sana.

Ziwa Nyasa ni moja kati ya maziwa yenye hadhi kubwa sana duniani, Afrika na Tanzania kwa ujumla, Ziwa hili katika makala mbalimbali za dunia limekuwa likishika nafasi kwanzia ya saba (7) hadi ya kumi (10) kulingana na makala husika kwa mfanothe times atlas of the world katika orodha yao wanasema ziwa hili ni la tisa (9) kwa ukubwa duniani, kutoka wikipedia ni ziwa la Tano kwa kuwa na kina kirefu sana duniani. katika tovuti ya 10most today ziwa nyasa limewekwa ni ziwa la tisa (9), katika tovuti ya fact monster ni ziwa la kumi (10)  na pia katika maps of the world ni ziwa la (8) kwa ukubwa duniani.

Katika afrika ziwa nyasa ni ziwa la tatu kwa ukubwa, baada ya ziwa Victoria, na Tanganyika chanzo ni wikipedia.

Pia ziwa Nyasa ni moja kati ya maziwa yenye sifa ya kuwa na aina nyingi za samaki ni (zaidi ya 1500


VIA-HOME OF TOURIST

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!