Monday 29 September 2014

MAJAMBAZI WAJERUHI POLISI, MFANYABIASHARA NA KUPORA MILIONI 30/=

WATU wawili akiwamo askari mmoja wamenusurika kifo baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, waliofanikiwa kupora mfuko wa fedha unaosadikiwa kuwa na zaidi ya shilingi milioni 30.




Tukio hilo, lilitokea jana mchana majira ya 8:30 katika Mtaaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi, ambapo majambazi hao walimvamia mmoja wa wafanya biashara wa Mchele hapa nchini aliyetambulika kwa jina la Salum Issa Suleiman (50), Mkaazi wa Baghani Mjini Unguja, ambaye walimpora mfuko wake wa fedha hizo wakati akiwa njiani kuzipeleka benki.



Mfanyabiashara wakati akiwa njiani alijikuta akizingirwa na mojaya gari ndogo na kuanza kushambuliwa kwa risasi ambazo zilimjeruhi sehemu zake za miguuni na ghafla 

kuanguka na ndipo majambazi hao walipowezakufanikiwa kumpora fedha hizo.



Wakati tukio hilo likitokea mmoja wa askari polisi wa Kituo cha Malindi Sajenti Hija Hassan Hija, alijaribu kupambana namabambazi hao, lakini alishindwa kufanikiwa baada na yeye kujeruhiwa sehemu ya mkononi na mguuni kutokana kushambuliwa kwa risasi.



Mfanyabiashara Salum alisema wakati alipokuwa akielekea maeneo ya Benki hiyo ndipo ilipotokea gari ndogo mbele yake na kumnadia mwizi na hapo ndipo walipompiga risasi ya mguu wa kulia na kumnyang’anya fedha hizo na kuondoka nazo.



Kwa upande wake askari Hija alisema, alipofika maeneo hayo ndipo alipomkuta Mfanyabiashara huyo akiwa katika harakati za kujinasua na hali na ndipo askari huyo alipokwenda kumuokoa lakini na yeye alishambuliwa na majambazi hao na kufanikiwa kuondoka na kitita hicho cha fedha zamfanyabiashara huyo.



Hata hivyo, majeruhi hao bado wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali kuu ya Mnazi mmoja na hali zao walieleza kuwa zinaendelea vizuri.



Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alisema ni kweli tukio hilo limetokea na aliyeporwa fedha hizo ni Mfanyabiashara wa Mchele katika maeneo ya Bandarini ambae alikuwa akielekea katika Benki ya PBZ tawi la Mlandege.



Alisema mfanyabiashara huyo alikuwa na fedha zenye thamani ya shilling milioni 30,6,00,000, ambazo ni mali ya tajiri wake anafahamika kwa jina la Yussuf Mohamed, ambazo alikuwa anakwenda kuziweka katika Benki hiyo.


Hata hivyo, Kamanda Mkadam, alitoa wito kwa Wananchi wakati wanapokwenda kuweka pesa kuacha kwenda kwa miguu na kuwatumia askari kwani askari wapo kwa ajili yao ili kuimarisha usalama wa raia.

Taarifa ya Tatu Makame, Laylat Khalfan    ZanziNews..

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!