Tumeshashuhudia baadhi ya waigizaji wa Bongo Movie ambao wamejaribu bahati zao upande mwingine wa sanaa kwa kujitosa kwenye muziki kama Shilole, na pia baadhi ya wasanii wa muziki kuamua kujitosa kwenye Bongo Movie.
Mwimbaji wa R&B Linah Sanga ameingia kwenye orodha ya wasanii wa muziki ambao wameanza kujihusisha na filamu, ambaye anatarajia kuonekana kwenye filamu mpya aliyocheza na Lulu.
Mwigizaji wa kike wa Bongo Movie ambaye alianza kuigiza akiwa na umri mdogo Elizabeth Michael aka Lulu anatarajia kuachia filamu mpya inayoitwa ‘Mapenzi Ya Mungu’, ambayo amecheza Linah.
Linah ameiambia Bongo 5 jinsi alivyopata nafasi ya kushiriki kwenye filamu hiyo ambayo ndio filamu yake ya kwanza kushiriki.
“Kipindi kile alichokuwa ametoka (Lulu),ametoka kama ana wiki mbili akanipigia simu akaniambia kuna movie nafanya na movie yenyewe nafikiri unaweza ukafanania na hiyo movie kulingana na kitu ambacho tumekiigiza humo ndani mambo mambo ya gospel imekaa kimambo mambo flani ya kidini dini kwa mbali kiaina”. Alisema Linah
No comments:
Post a Comment