OFISA Elimu Shule za Sekondari wilayani Temeke Dar es Salaam, Donald Chavilla amesema kukosa elimu ni sawa na kibatari.
Alisema hayo mwishoni mwa wiki katika mahafali ya tisa ya kidato cha nne iliyohusisha wahitimu 128 katika shule ya sekondari Pius iliopo Kongowe jijini Dar es Salaam.
“Hakuna njia ya kufaulu ila kusoma kwa bidii, walimu fundisheni wanafunzi kwa upendo wafikie malengo yao, kumbukeni ualimu ni wito na anayesema sio aondoke… kuna kazi nyingi zaidi ya kufundisha,” alisema Chavilla.
Mkuu wa shule hiyo, Lucas Hassan alisema shule yao imenunua vifaa vingi na kemikali za kutosha kwa ajili ya wanafunzi kujifunza kwa vitendo na kuwajengea uwezo wa kufanya vizuri katika mitihani yao.
Akitoa nasaha kwa wahitimu, alisema mwanafunzi akitumia muda wake vizuri kwa kujisomea itamsaidia kufaulu mtihani wake
1 comment:
sawa ni kweli asemalo lakini yapasa waangalie na mifumo yetu ya elimu hafukuzani kabisa na mabadili ya kiteknolojia
Post a Comment