Nembo ya Dira ya Jukwaa la Katiba Tanzania.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata) Deus Kibamba (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mambo muhimu ya kuzingatiwa baada ya makubaliano ya kuahirisha mchakato wa Katiba Mpya baada ya Uchaguzi Mkuu 2015. Kushoto ni Mratibu wa Mtandao wa Mapambano ya Ukimwi kwa Wanaume Tanzania (WOFATA), Alex Margery. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu 0712-727062)
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata) Deus Kibamba (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mambo muhimu ya kuzingatiwa baada ya makubaliano ya kuahirisha mchakato wa Katiba Mpya baada ya Uchaguzi Mkuu 2015.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata) Deus Kibamba (wa pili kulia) akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Mratibu wa Jukata, Diana Kidara, Mratibu wa Mtandao wa Mapambano ya Ukimwi kwa Wanaume Tanzania (WOFATA), Alex Margery na Mjumbe wa Bodi kutoka Shirikisho la Vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (Shivyawata), Maria Chale.
Wapiga picha wa vyombo vya habari wakichukua tukio hilo.
Dotto Mwaibale
JUKWAA la Katiba Tanzania (Jukata) limesema iwapo Bunge maalumu la Katiba litaendelea mjini Dodoma baada ya mchakato wake kusitishwa kupisha uchaguzi mkuu wa 2015 watakwenda kufunga kwa kufuri milango ya jengo hilo ili kuokoa fedha za watanzania zinazotumika vibaya kwa kulipana posho.
Katika hatua nyingine Jukata limetangaza jimbo la uchaguzi la Samueli Sita kuwa lipo wazi na nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Fredirick Werema kuwa wazi baada ya kuwatuhumu kuchangia kwa kiasi kikubwa kuharibu mchakato huo wa katiba mpya.
Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mambo muhimu ya kuzingatiwa baada ya makubaliano ya kuahirisha mchakato wa Katiba Mpya baada ya Uchaguzi Mkuu 2015
“Nafasi za Sita na Werema tunatangaza kuwa sasa zipo wazi baada ya kupoteza sifa za kuongoza kufuatia kuvuruga mchakato wa katiba mpya na kuwa katika kipindi cha miaka 10 hawatakiwi kugombea nafasi yoyote katika nchi hii hata iwe ya mjumbe wa shina” alisema Kibamba.
Kibamba alivipongeza vyama vya siasa vilivyochini ya Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kwa makubaliano yaliyofanyika na Rais Jakaya Kikwete Agosti 8 mwaka huu Ikulu ndogo ya Chamwino Dodoma kuwa ni ya faraja na matumaini makubwa kwa taifa.
Alisema kutokana na mazungumzo hayo imekubalika kuwa mchakato wa Katiba mpya uahirishwe kwa sasa hadi baada ya uchaguzi Mkuu wa 2015.
Akizungumzia kuhusu kufunga milango ya jengo la Bunge ili asiingie mtu alisema hilo litafanyika baada wiki mbili kuanzia leo iwapo tu wabunge hao wataendelea na mchakato wa katiba hiyo na kuwa tukio hilo watalifanya kwa umoja wao.
Kibamba aliongeza kuwa kutokana na masuala ya Katiba kuwa na unyeti kwa taifa zima na kwa jinsi yanavyoshikamana na masuala ya uchaguzi ambayo nayo yana wadau wengi nje ya wanasiasa Jukata wanaona kuna haja ya kupanua wigo wa mazungumzo na makubaliano yanayoendelea na yatakayokuja siku na miezi ijayo yawe kwa taifa zima na si kwa wanasiasa.
“Jukata pia tunapongeza uamuzi wa wanasiasa kuahirisha uchaguzi wa serikali za mitaa uliokuwa ufanyike mwezi Septemba 2014 mpaka mwaka 2015 hata hivyo zipo hoja za msingi kuhusu uchaguzi huo” alisema Kibamba.
No comments:
Post a Comment