Friday 26 September 2014

INAKISIWA ZAIDI YA RAIA 3000 KUTOKA ULAYA NI WAFUASI WA ISLAMIC STATE


Inakisiwa kuwa zaidi ya raia 3000 kutoka Ulaya ni wafuasi wa Islamic State



Idadi ya raia kutoka Uropa wanaojiunga na kundi la wapiganaji wa Kiislamu nchini Syria na Iraqi imeongezeka hadi zaidi ya 3,000 kulingana na mkuu wa kitengo cha kupambana na ugaidi bara la ulaya.
Gilles de Kerchove ameonya kuwa mashambulizi ya hewa yanayofanywa na nchi za Magharibi yataongezea hatari ya mashambulizi ya kulipiza kisasi katika bara la Ulaya.
Vikosi vikiongozwa na Marekani vimetekeleza mashambulizi ya hewa mia mbili dhidi ya wanamgambo wa Islamic state wa Iraqi tangu Agosti na Jumatatu iliyopita wakaanza kulenga wale walioko Syria.
Bunge la Uingereza litapiga kura kwa mashambulizi ya hewa dhidi ya Iraqi siku ya Ijumaa.
Kundi la IS wameteka sehemu kubwa za Syria na Iraqi katika miezi ya hivi karibuni.
CIA inakisia kuwa kundi la IS linaweza kuwa na wapiganaji mpaka 31,000 huko Iraq na Syria, mara tatu zaidi ya wale waliohofiwa.

CIA inakisia kuwa Islamic State inazaidi ya wafuasi 30,000

Mashambulizi haya yaliotekelezwa siku ya Alhamisi na ndege za Marekani, Saudi na UAE zilikuwa zinalenga mitambo 12 ya kusafisha mafuta nchini Syria .
Msemaji wa Pentagon Rear Admiral John Kirby alisema kuwa kusudi la mashambulizi haya ya hewa halikuwa kuwaua wanamgambo hao lakini ilikuwa kuharibu maeneo ambayo yalikuwa yakiletea kundi hilo fedha kupitia soko nyeusi.
Baadaye, siku ya Ijumaa, wabunge wa Uiungereza wataulizwa kuunga mkono mashabulizi dhidi ya wanamgambo wa IS Iraqi lakini sio Syria.

BBC-SWAHILI

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!