Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo ambao ni Waandishi wa Habari mkoani Mara Frolence Focus wa Mwananchi na Pendo Mwakembe wa Raia Tanzania wamenusurika kwenye ajali hiyo wakiwa kwenye basi la Mwanza Coach kutokea Musoma
Eneo la ajali
wananchi waliofika eneo la tukio
Uokoaji wa gari dogo ukiendelea Gari dogo lililotumbukia mtoni baada ya kuondolewa mtoni |
Inaelezwa kuwa ajali hiyo imehusisha magari matatu na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 30 na kujeruhi watu zaidi ya 70 katika eneo la Sabasaba wilayani Butiama.
Akizungumzia kwa tabu akiwa amelazwa kwenye wodi namba 4 hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mra, Frolence amesema walishangaa kuona abiria waliokuwa wamekaa mbele wakisimama na kurudi nyuma na ghafla akasikia mlio mkubwa. Bas likiwa limeharibika vibaya sehemu ya mbele Mashuhuda Wamesema mabasi hayo ambayo yote yalikuwa kwenye mwendo kasi yalikutana kwenye daraja dogo katika eneo hilo huku pia gari dogo aina ya Land Crusser likitaka kuovateki na hivyo kupelekea kutokea kwa ajali hiyo. Mmoja wa mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa jina la Juma Nyamhanga amesema alisikia kishindo kikubwa muda mfupi baada ya kutokea kwa ajali hiyo na baadae kusikia vilio vikitokea ndani ya mabasi hayo. |
Miili ya watu waliofariki katika jali ya mabasi ya Mwanza Coach na J4 Express eneo la sabasaba wilayani Butiama mkoani Mara,waliofariki ni zaidi ya 30,majeruhi zaidi ya 70
Mabasi yakiwa yamegongana
Wananchi wakiangalia bas la Mwanza Coach Ndani ya moja ya mabasi hayo |
Ajali hii imetokea majira ya saa 5 na nusu ,Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara
Kufuatia ajali mbaya iliyohusisha magari matatu wilayani Butiama mkoani Mara
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Butiama Anjelina Mabula aliyezungumza na TBC muda mfupi uliopita amesema idadi ya watu waliopoteza maisha ni 38 hadi sasa huku majeruhi wakiwa ni 80.
Amesema ajali hiyo imehusisha basi la AM Coach lenye namba za usajili T736 AWJ likitoka Musoma kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi T677 CYC J4 Express likitoka Mwanza kwenda Tarime na gari jingine dogo aina ya Nissan Corola P332 KKT likitoka eneo la Sabasaba yote yalikutana kwenye mteremko yakitokea juu kwenda Darajani ,katika kupishana kutokana na spidi yao hawakuweza kupishana yakagongana na wakati huo gari hilo dogo lilipaki pembeni baada ya kuona hali tete nalo likagongwa kwa nyuma likasukumwa na kutumbukia mtoni.
Katika gari dogo kulikuwa na watu 8,wawili wamefariki dunia na majeruhi 36 kutoka kwenye mabasi hayo mawili nao wamefariki na majeruhi 80 wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Mara.
Madereva wote wamefariki dunia katika ajali hiyo mbaya
SOPHIEMBEYU BLOG INATOA POLE KWA WOTE WALIOPOTEZA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI KATIKA AJALI HII YA KUTISHA. MUNGU AWALAZE MAREHEMU WOTE MAHALI PEMA PEPONI ..
No comments:
Post a Comment