Wananchi wa Lupingu Ludewa wakilitazama daladala lililopata ajali na kusababisha kifo cha aliyekuwa diwani wa viti maalum kata ya Lupingu Prisca Kayombo leo
Diwani wa viti maalum Lupingu Prisca Kayombo(Zaruta) akishiriki kubeba nguzo ya umeme |
Diwani wa viti maalum Lupingu Prisca Kayombo(Zaruta) kulia akishirikiana na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kufukia nguzo za umeme kwenda kata ya Lupingu katika kijiji cha Ntumbati wiki mbili kabla ya kifo chake leo
Gari ya wagonjwa ikiwashusha majeruhi katika Hospitari ya wilaya ya Ludewa waliokuwamo katika ajari
majeruhi wakishushwa hospitari
Wananchi wa kata ya Ludewa wakishuhudia majeruhi waliokuwa wakishushwa katika gari ili kuwatambua
Habari na picha na Matukiodaima.co.tz
DIWANi wa viti maalum kata ya Lupingu wilaya ya Ludewa Prisca Kayombo(Zaruta) amekufa papo hapo na wengine kujeruhiwa vibaya katika ajali ya ajali mbaya ya gari iliyotokea leo asubuhi.
Mashuhuda wa ajali hiyo waliozungumza na mtandao huu walidai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni gari hilo ambalo walikuwa wakisafiriki kutoka Lupingu – Ludewa kufeli breki na hivyo kupinduka .
Credo Haule alisema kuwa baada ya gari hilo aina ya Toyota Costa inayojulikana kwa jina la DMX iliyokuwa ikifanya safari zake kutoka Ludewa Mjini kuelekea Lupingu ,kufeli breki dereva aliwataka abiria kutulia ndani ya gari hilo ila diwani huyo hakuweza kufanya hivyo na kuamua kuchukua maamuzi magumu ya kutaka kuruka katika gari hilo.
Alisema kuwa wakati akiruka alimsukuma utingo wa basi hilo na hivyo wote wawili utingo na diwani kufunikwa na gari hilo na kupelekea kifo cha diwani huyo huku utingo huyo akiwa mahututi baada ya kubanwa na gari hilo.
” Diwani huyo amepoteza maisha wakati akiwa njiani kuelekea kujumuika na wananchi wake katika shughuli ya maendeleo ya kuchimba mashimo ya nguzo za umeme kuelekea kijijini kwake Lupingu”
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe ameeleza kusikitishwa na kifo cha diwani huyo kutokana na mchango wake mkubwa aliouonyesha enzi wa uhai wakati kwa kushiriki vema na wananchi wa kata yake katika zoezi la kufyeka na kuchimba mashimo ya nguzo za umeme kwenda Lupingu.
Alisema kuwa anakumbuka ni wiki mbili pekee zimepita toka diwani huyo alipoungana nae katika uchimbaji wa mashimo ya nguzo za umeme kwenda kijiji cha Ntumbati na kuwa hata wakati ajali hiyo inamkuta bado alikuwa katika harakati za kuwatumikia wananchi wake.
” Ludewa tumempoteza diwani mchapa kazi na aliyependa kujituma muda wote na hata wakati mwingine diwani huyo alikuwa akifanya kazi ngumu kama mwanaume kwa kubeba nguzo za umeme kwa kushirikiana na mimi na wananchi wake …..kwweli kifo chake ni pigo kubwa ndani ya CCM na kwa wananchi wa kata nzima ya Lupingu”
Kwani kati ya madiwani waliokuwa bega kwa bega na wananchi wao na mbunge ni pamoja na diwani huyo ambae alikuwa mstari wa mbele kuona kata ya Lupingu inapata umeme wa uhakika baada ya miaka zaidi ya 50 ya Uhuru bila umeme .
Mbunge Filikunjombe alisema atamkumbuka diwani huyo kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo na vile alivyofanya kazi na wananchi wote bila kujali itikadi zao za vyama.
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyosababisha kifo cha diwani huyo na kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 2 asubuhi
1 comment:
aziz bilal02:17
1
Reply
Sasa watu kufariki kwa ajali za usafiri wa mabasi nchini imekuwa kama jambo la kawaida,madereva wa buses wawe wanachunguzwa kama ni alcoholics au wavutaji wa dawa za kulevya.
Post a Comment