Hii ndio taarifa iliyochapishwa dakika chache zilizopita katika ukurasa rasmi wa Yanga katika mtandao wa kijamii wa Facebook.
KUMRADHI:
Wapenzi, wanachama, washabiki na wadau wa soka kwa ujumla,
Mechi kati ya Young Africans dhidi ya Big Bullets iliyokua ifanyike leo haitakuwepo.
Kwa mujibu wa waandaji wa mchezo huo DRFA timu ya Big Bullets imeshindwa kuwasili nchini, na jitihada za kupata timu nyingine imeshindikana.
Tunawaomba radhi kwa usumbufu wote ambao umejitokeza.
Daima Mbele Nyuma Mwiko
No comments:
Post a Comment