Thursday, 18 September 2014

AUAWA KWA TUHUMA ZA KUIBA BAISKELI

Mwili wa Marehemu Lugano  Pembezoni mwa Barabara


Mtu mmoja aliyefahamika kwa majina ya Lughano John aliye na miaka 36 mkazi wa Ipinda Juu ameuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na wananchi wenye hasira kali walioamua kujichukulia sheria mkononi baada ya marehemu kutuhumiwa kuwa ameiba baiskeli. (FS)

Tukio hilo limetokea jana asubuhi ya saa nne katika kitongoji chaLutusyo, kijijini Talatala katika Tarafa ya Ntebela wilayani Kyela mkoani hapa Mbeya.
Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio zinaeleza kwamba 
 
Marehemu Lughano John alikamatwa na wananchi hao akiwa na baiskeliya wizi na kisha kuanza kumshambulia kwa kumpiga hali iliyopelekea kifo chake.Wakati msako wa kuwatafuta watu waliohusika na tukio hilo ukiendelea, Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi amethibitishia Fichuo Tz kutokea kwa tikio hilo na  kutoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake wawe na tabia ya kuwapeleka watuhumiwa wanaokwamatwa katika mamlaka husika.

1 comment:

Anonymous said...

aziz bilal03:35


1
Reply

Hatari sana hii tabia ya kuuwana namna hiyo,yaani mtu anauwawa njiani na kuachwa mpaka watoto wadogo wanamuona mtu amekufa barabarani,umri wa hawa watoto pichani ni mdogo sana kushuhudia kitendo kama hicho.

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!