Tuesday 23 September 2014

ALIYEUA MKE KWA WIVU NAYE AUAWA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime
WATU wenye hasira wamempiga hadi kumuua mwanamume, aliyemuua mke wake kwa kumpiga rungu tumboni.



Kamanda wa Polisi mkoani hapa, David Misime, alisema tukio hilo la Septemba 20, mwaka huu katika Kijiji cha Mzogole wilayani Mpwapwa, ambapo mtu mmoja, Mwajuma Chomola (48) aliuawa kwa kupigwa na rungu tumboni upande wa kushoto na mume wake, Richard Kodi (55).
Hata hivyo, alisema Kodi naye aliuawa Septemba 21, mwaka huu baada ya kushambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi. Alifariki dunia akiwa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa.
Aliuawa baada ya wananchi hao kupata taarifa kuwa mwanamke huyo, amekufa baada ya kupigwa na mtu huyo.
Misime alisema uchunguzi wa awali, unaonesha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi.
Kamanda huyo alisema Kodi alimuua mkewe huyo, aliyekuwa akiishi naye baada ya kuchelewa kurudi kutoka kwenye sherehe, iliyokuwa kijijini hapo, akidhani kuwa alikuwa ameenda kwenye masuala mengine.

1 comment:

Anonymous said...

1


Jino kwa jino!fair justice!

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!