Monday, 25 August 2014

WANAJESHI WANNE WA NEPAL AKIWEMO PIA KOMANDO WAO WAKAMATWA NCHINI MUDA HUU BILA KIBALI


Wanajeshi hao wa jeshi la nchi ya NEPAL wakiwa wanaonyesha vyeti vyao vya uanajeshi wa jeshi hili


        Idara ya uhamiaji Jijini Dare s salaam imewakamata raia 12 wa kigeni waliokuja nchi kinyume na sheria wakiwemo wanajeshi wanne wa  jeshi la NEPAL pamoja na nane kutoka nchini india walioletwa nchini kinyume na sheria kwa kisingizio cha maisha magumu nchini kwao.
  
     Raia  hao wamekamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya ESCOT iliyoko kijitonyama jijini Dar es salaam katika operation maalum iliyoendeshwa na idara ya uhamiaji Jijini baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi wa maeneo hayo juu ya uwepo wa watu hao ambao waliwatilia mashaka.

Afisa uhamiaji wa jiji la Dar es salaam GRACE HOKORORO akizungumza na mtandao huu kuhusu sakata hilo
         Wanajeshi hao wanne wa jeshi la NEPAL yumo pia komando mmoja wa jeshi hilo ambao nao wamedai kuletwa nchini kwa ajili ya kutafutiwa ajira ya maswala ya ulinzi katika nchi za Africa hivyo wakashukia Tanzania kama kituo kwa ajili ya kufanikisha malengo yao.

        Akizungumza na mtandao huu muda mfupi uliopita afisa wa uhamiaji wa jiji la Dar es salaam GRACE HOKORORO amesema  kuwa wahamiaji hao wamekuwa wakipita katika nchi ya Tanzania na kupelekea nchi nyingine kama Africa ya kusini  kwa ajili ya kufanyishwa kazi zisizo halali



Picha mbili zikionyesha wanajeshi hao wakiwa katika nchi yao wakiwa wanalitumikia jeshi la nchi yao kabla ya kutimka na kuja nchini
      Aidha amesema kuwa watu hao wamekuwa wakiletwa na mawakala ambao wamekuwa wakiwatoa katika nchi zao kwa ahadi  la kuwatafutia kazi katika nchi hizi jambo ambalo amesema kuwa linatafsiriwa kama biashara ya binadamu ambapo mawakala waliowaleta watu hao hadi sasa hawajapatikana.
          
         Aidha Bi GRACE amewataka watanzania na watu wasamaria wema kuwafichia watu wanaowaficha watu kama hao kwani ni kinyume na sheria na baadae huleta madhara makubwa kama uhalifu na uuzwaji wa madawa ya kulevya

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!