Wednesday, 13 August 2014
UKATILI HUU MPAKA LINI!! BABA ADAIWA KUMPIGA MWANAE HADI KUFA HUKO MOSHI
Mtoto wa miaka minne (jinsia ya kiume) ambaye alikuwa akiishi Moshi mjini amefanyiwa ukatili na kupigwa na baba yake mzazi hadi kufariki dunia, sababu haswa ya baba yake huyo kumpiga na hadi kumsababishia umauti mwanaye huyo bado haija fahamika. KITAANI BONGO NEWS iliongea na msamaria mwema mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe ambaye pia alikuwa ni shuhuda wa tukio hilo alielezea tukio hilo kwa uchungu huku akibubujikwa na majonzi makubwa. Hata hivyo, hatukuweza kupata jina la mtoto huyo na mzazi wake kwa sasa, endelea kufatilia tukio hili tunaendelea kuwajulisha kwa kina kila kinachoendelea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment