Saturday 2 August 2014

SERIKALI YACHIMBA VISIMA 79 VYA UTAFUTAJI GESI

SERIKALI imesema hadi sasa tayari imechimba visima vya utafutaji mafuta na gesi asilia 79 sawa na asilimia 37 ya kazi hiyo.

Hayo yalielezwa jana na Kaimu Mkurugenzi Mkakati na Mipango wa Shirika la Maendeleo na Petroli (TPDC), Dk. Wellington Hudson katika semina ya siku mbili kwa waandishi wa habari iliyoandaliwa na shirika hilo.
Alisema kwa hatua hiyo, ni mafanikio makubwa ukilinganisha na nchi nyingine zinazotunguka.
Dk. Willington, alisema visima hivyo vya gesi viko Mnazi Bay, Mkuranga, Songosongo, Ntoria na Kiruani.
Alisema gesi hiyo imetoa matumaini makubwa kwa wananchi na serikali, kutokana na kuchangia pato kubwa la taifa kutokana na matumizi ya majumbani na viwandani

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!