Watuhumiwa hao walikamatwa mnamo tarehe 04/8/2014 wakiwa na noti bandia zipatazo 10,640 za dola mia (100) ambazo ni sawa na dola 1,064,000 ambazo ni zaidi ya shilingi za Kitanzania bilioni moja katika nyumba namba 07 walimokuwa wamepanga.
Polisi walipata taarifa kutoka kwa wananchi na kuweka mtego ambapo askari walifika katika eneo hilo na kuwatia mbaroni watuhumiwa wakiwa na noti hizo bandia zilizokuwa zimefungwa mabunda themanini na kasiki ndogo ambayo imefungwa kwa namba za siri. Aidha watuhumiwa walikiri kujihusisha na utengenezaji wa noti bandia.
1.AHMAD S/O MOHAMED Miaka 50, mfanyabiashara, mkazi wa Mombasa Kenya
2.RICHARD S/O MAGOTI Miaka 61, mfanyabiashara, mkazi wa Musoma mkoani Mara.
3.SIMONI S/O LUKIKO Miaka 58, mkazi wa Magomeni Kagera
4.HUMPHREY S/O LEONARD Miaka 34, mlinzi, mkazi wa Mburahati
5.FRANK S/O CHARLES Miaka 31 mfanyabiashara, mkazi wa Sinza
6.ABDALLAH S/O YUSUPH, Miaka 34, mfanyabiashara, Mkazi wa Sinza
7.BAKARI S/O BAKARI, Miaka 31, mfanyabiashara, mkazi wa Mbezi, Kimara.
Watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
No comments:
Post a Comment