Thursday, 14 August 2014

NAIBU WAZIRI MASELE AWATAKA VIJANA KUJIKITA KATIKA MAMBO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

m1
Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen Masele (kulia) akimkabidhi zawadi Kijana Mwanasayansi Duniani toka nchini India wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

m2
Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen Masele (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Vijana Wanasayansi Duniani wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere. Wa kwanza kulia ni Makamu Mwenyekiti na Mwakilishi wa Vijana Wanasayansi Duniani (YES) na anaemfuatia ni Rais wa YES Bw. Meng Wang. Wa kwanza toka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania, Profesa Abdulkarim Mruma akifuatiwa na Rais wa Wajiolojia Afrika Profesa Aberra Mogessie.
m3
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi na Mwakilishi wa Vijana Wanasayansi Duniani Bw. Stephen Nyagonde wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa ufungaji wa Kongamano hilo.
m4
Rais wa Vijana Wanasayansi Duniani Bw. Meng Wang akitoa maelezo machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
m5
Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen Masele akiwahutubia Vijana Wanasayansi Duniani wakati alipokuwa akifunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
m7
Baadhi ya Vijana Wanasayansi Duniani waliohudhuria siku ya ufungaji Kongamano wakifuatilia kwa makini hotuba ikiyotolewa na mgeni rasmi wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
m8
Baadhi ya Vijana Wanasayansi Duniani waliohudhuria siku ya ufungaji Kongamano wakifuatilia kwa makini hotuba ikiyotolewa na mgeni rasmi wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
PIX
Rais wa Vijana Wanasayansi Duniani (YES), Bi. Elyvin Nkhonjera kutoka nchini Malawi akikaribisha wageni waalikwa wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
……………………………………………………………………………………………………
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
 
NAIBU Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele amewataka vijana nchini kupenda kujikita katika masomo ya sayansi na teknolojia kama mihimili yenye kuleta maendeleo kwa haraka ulimwenguni ili waweze kupata ujuzi na mitazamo katika sekta ya gesi ambayo inakuwa kwa kasi kubwa nchini.
 
Mhe. Masele ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akifunga Kongamano la Tatu la Vijana Wanasayansi Duniani lililofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, kongamano ambalo liliwakutanisha vijana toka nchi zaidi ya 46 ulimwenguni zikiwemo baadhi ya nchi za Afrika ambapo Tanzania ilikuwa mwenyeji wa Kongamano hilo.
 
Mhe. Masele ameeleza kuwa sayansi na teknolojia ndiyo mihimili mikubwa ya sasa katika kuleta maendeleo ya haraka katika nyanja mbalimbali kwani mambo mengi hivi sasa hutegemea sayansi na teknolojia.
 
Aidha, Mhe. Masele amezitaja baadhi ya changamoto zinazozikabili baadhi ya nchi za Afrika katika kupata maendeleo ni pamoja na kutowekeza katika sayansi na teknolojia hali inayopelekea baadhi ya nchi nyingi kukosa wataalam wa kutosha katika mambo ya sayansi na teknolojia, hivyo amezitaka nchi za Afrika kuwekeza katika sayansi ili kuweza ili kubadilisha uchumi wa Afrika.
 
“Sayansi na teknolojia huleta maendeleo makubwa hivyo nawapa moyo vijana muendelee kufanya kazi kwa bidii na kujituma katika mambo ya sayansi na teknolojia ili muweze kuleta uchumui endelevu”. Alisema Masele.
 
Akizungumzia kwa upande wa Serikali ya Tanzania, Mhe. Masele amesema kuwa serikali ya Tanzania imewekeza nguvu zake kwa sasa katika kuendeleza sayansi ya afya kwa kuanzisha Vyuo mbalimbali na kuwasomesha watanzania nchi mbalimbali za nje ili waweze kwenda kupata ujuzi na kuwa wataalam na wakaguzi katika sekta ya gesi pamoja na mafuta kwa lengo la kuja kuisaidia nchi yao.
“Wajibu wetu kama Serikali tumeamua kwa makusudi kusomesha vijana katika nchi mbalimbali ili wakaweze kupata elimu juu ya sayansi na teknolojia hasa katika masuala ya gesi ili kupata wataalam na wakaguzi wa kutosha nchini ambao watalisaidia taifa kuinua uchumi wake na hivi sasa serikali imeanzisha vyuo mbalimbali nchini, program mbalimbali za mafunzo kwa watanzania, imetoa ufadhili wa masomo kwa watanzania na imedhamini makongamano ya vijana ili wapate fursa ya kujiendeleza.” Alisisitiza Masele.
Mhe. Masele amempongeza Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo kwa kazi kubwa anayoifanya katika Wizara yake na pia amewapongeza vijana waliohudhuria katika kongamano hilo pamoja kuyapongeza Makampuni wadhamini wa kongamano hilo na kuyataka makampuni hayo kuendelea kuwekeza pamoja na kulipa kodi ili serikali iweze kukusanya mapato na wananchi wapate kunufaika na mapato hayo.
Naye Rais wa Vijana Wanasayansi Duniani (YES) Bw. Meng Wang amemshukuru Makamu wa Rais wa Tanzania, Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Naibu Waziri steven Masele kwa kuwaunga mkono vijana waliohudhuria kongamano hilo na kuonesha hali nzuri ya ushirikiano baina ya serikali na vijana na amewaasa vijana kujikita katika sayansi na teknolojia kama mihimili mikuu ya maendeleo duniani.
“Naishukuru sana Tanzania pamoja na ujio wa Mawaziri wake katika kufanikisha kongamano hili la vijana wanasayansi, nawashukuru pia wadhamini wa makampuni mbalimbali wa kongamano hili pamoja na vijana kwa ujumla toka nchi mbalimbali duniani”. Alisema Wang

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!