Mazishi ya mwanafunzi aliyeuawa kikatili kwa kubakwa kisha kutobolewa macho na watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa kichakani katika kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga yamefanyika katika makaburi ya familia katika kijiji cha Negezi kata ya Mwawaza katika manispaa ya Shinyanga.
Mwanafunzi huyo aliyekuwa anasoma darasa la tatu katika shule ya Msingi Negezi iliyopo kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga alikutwa ameuawa kwa kubakwa kisha kutobolewa Agosti 25 mwaka huu saa saba mchana katika kitongoji cha Kashampa kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi.
Akizungumza wakati wa mazishi ya mwili wa marehemu yaliyofanyika LEO MCHANA naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila alilaani kitendo cha kinyama alichofanyiwa mtoto huyo huku akiitaka jamii kushirikiana na jeshi la polisi katika kuwafichua wahusika wa mauaji hayo.
“Kifo cha mtoto huyu ni mapenzi ya mungu yaliyosababishwa na wanadamu wabaya,naomba suala la hili lifuatiliwe hatuhitaji siasa katika hili inauma sana kwani vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinatishia amani Shinyanga”,alieleza Nkulila.
Kwa upande wake Intelijensia mkoa wa Shinyanga Bundala Maige alisema suala la ulinzi kwa watoto ni jamii nzima na kwamba wahalifu wako ndani ya jamii hivyo kuitaka jamii kuwafichua wahalifu hao ili kukomesha vitendo vya ukatili vinavyoendelea mkoani Shinyanga.
Naye mwenyekiti wa mtaa wa Masekelo kata ya Masekelo yalikofanyika mazishi ya mtoto huyo bwana Peter Juma Kitundu alisema kifo cha mtoto huyo kinatia simanzi kubwa kwani kimesababishwa na binadamu huku akiiomba serikali kulifanyia uchunguzi wa kina tukio hilo na lisiingizwe suala la siasa.
Kwa upande wake mwinjilisti Emmanuel Donald Kaswalala aliyeendesha ibada ya mazishi alilaani vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watotot huku akiiomba jamii kumrudia mwenyezi mungu kwa kuondokana na matendo mabaya
No comments:
Post a Comment