Saturday 23 August 2014

MHOLANZI MBARONI KWA KUSAFIRISHA WATU

Raia wa Uholanzi mwenye asili ya Iraq, Hirwan Naseh Ismail akiwa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji jana, akisubiri kusafirishwa baada ya kufukuzwa nchini akituhumiwa kujihusisha na mtandao wa usafirishaji wa wahamiaji haramu, kushoto kwake ni Ofisa Uhamiaji Halid Marusu.  Picha na Beatrice Moses


Idara ya Uhamiaji nchini imefanikiwa kumkamata mtu anayeshukiwa kuhusika na mtandao wa usafirishaji wa wahamiaji haramu kutoka mataifa ya Syria, Iran na Iraq kwa kutumia hati bandia za kusafiria.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwa niaba ya msemaji wa idara hiyo, ofisa wa idara hiyo Tatu Burhan alimtaja mtu huyo kuwa ni Shirwan Naseh Ismail ambaye ni raia wa Uholanzi mwenye asili ya Iraq, ambaye amefukuzwa nchini na kumzuia kuingia tena.
Alisema kuwa mtuhumiwa huyo ataondoshwa nchini leo kwa hati ya kufukuzwa yenye namba 0054217( P.I notice), kwa ndege aliyokuja nayo.
“ Alikamatwa Agosti 21 saa 8. 35 akijaribu kuingia nchini kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uturuki yenye namba 603. Shirwan ni miongoni mwa washukiwa wa mtandao wa kusafirisha wahamiaji haramu kwa kutumia hati bandia za mataifa mbalimbali ya Ulaya,” alisema Burhan.
Alisema kuwa alipopekuliwa alikutwa na fedha nyingi za kigeni za mataifa mbalimbali, pia chakula kingi kilichopikwa akiwa amekihifadhi katika hali inayoonyesha hapendi kula kwenye hoteli kwa nia ya kujificha.
Alisema maofisa uhamiaji baada ya kufanya uchunguzi, walibaini kuwa Shirwan amekuwa akiingia nchini mara kwa mara kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) na kutoka kupitia mpaka wa Tunduma, Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro na Zanzibar.
Burhan ambaye pia ni Ofisa Uhusiano wa Uhamiaji, alieleza kuwa wakati Shirwan alipokamatwa alikuwa ameambatana na raia watano wa Iraq, waliotumiia hati za kusafiria za Uguriki, ambapo baada ya ukaguzi wa kina iligundulika kuwa hati hizo ni bandia,” alisema.
Burhan alisema kuwa watu hao hawakuruhusiwa kuingia nchini na wawili kati yao tayari wamerudishwa walikotoka huku wengine watatu wakizuiliwa na Idara ya Uhamiaji, uwanjani hapo wakati wakisubiri kurudishwa nchini Uturuki walikotokea.
“Juhudi za uhamiaji kupamba na uharamia wa kiuhamiaji zitaendelea usiku na mchana hadi kuuzima kabisa mtandao huu uliojitokeza hivi karibuni. Pia tunawaonya raia na wageni wanaojihusisha na biashara hiyo haramu. Tunaomba ushirikiano kwa wananchi ili kupambana na uhalifu huu,” alisema Burhan.
TZ-DAIMA

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!